Chai FM

Mbwa wageuka tishio kata ya Lyamkena Makambako

1 October 2026, 1:17 pm

Baadhi ya wananchi wakiwa na mbwa zao wakati wa zoezi la uchanjaji wa mbwa wao (Picha na Cleef Mlelwa)

Watoto wengi walioripotiwa kudhurika na mbwa mtaa wa Lyamkena Makambako Tanzania ni kutokana na uzembe wa wamiliki wa mbwa hao.

Na Cleef Mlelwa

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Ilangamoto  uliopo kata ya Lyamkena  halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe ,Jailosi kadaga,Levi Nyamle na Jema Kitumbika wakizungumza na mwandishi wetu katika  maadhimisho ya siku ya  kichaa cha Mbwa ambayo yamefanyika mtaani hapo,ambapo wamesema wafugaji wengi wanafuga Mbwa kwa mazoea kutokana na  kushindwa  kuihudumia hali inayopelekea mifugo hiyo izurure mtaani ili kujitafutia chakula.

Sauti za wananchi wakieleza changamoto za mbwa mtaani

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ilangamoto Naboti Kiwale amesema  kumekuwa na changamoto kubwa ya mbwa kuzurula katika mtaa wake,hali inachangiwa na mwenye mbwa kutowahudumia na kusababisha adha kwa watoto,huku akitaka elimu zaidi kuendelea kutolewa.

Sauti ya mwenyekiti akizungumzia uwepo wa kero hiyo

Akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho hayo afisa mifugo  halmashauri ya mji wa Makambako Samson Mgaya amesema kwa mwaka huu 2026  hadi kufikia mwezi wa nane watu sita wameng’atwa na Mbwa,Ng’ombe nane, na mbuzi mmoja,huku mwaka 2025 watu 10 wakiripotiwa kung’atwa na Mbwa.

Sauti ya afisa mifugo wa halmashauri akisoma taarifa

Afisa mifugo halmashauri ya mji wa Makambako Samora Mgaya amewataka wafugaji wa mbwa kuhakikisha wanatoa wanyama hao wanapatiwa chanjo kwa wakati,huku akitaja hatua za awali ambazo mbwa mwenye kichaa huzionyesha ikiwemo kupoteza hamu ya kula,kupenda kujitenga,kuwa mpole na wasiwasi.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Salumu Mlumbe ametaka wataalamu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ufugaji bora wa Mbwa huku akitaka wafugaji wote wa Mbwa  wanapata  chanjo.

Maadhimisho ya kichaa cha Mbwa yameongozwa na kauli mbiu inayosema Tuna Nguvu, tukiwa pamoja, ambapo halmashauri ya mji wa Makambako imeadhimisha kwa kuchanja bure Mbwa 172 na kutoa elimu kwa wananchi na wanafunzi namna ya kukabuliana na ugonjwa wa kichaa cha Mbwa