Chai FM

Madawa ya kulevya chanzo ukatili wa wanawake na wasichana Rungwe

25 November 2026, 12:33 pm

Imani potofu na matumizi ya madawa ya kulevya ni miongoni mwa sababu zinazosababisha wanawake wengi na wasichana kufanyiwa ukatili wa kijinsia katika jamii.

Picha ya pamoja ikionesha washiriki wa kikao kazi cha watetezi wa haki za wanawake na wasichana kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali. Picha na Sabina Martin

Na, Sabina Martin

Imeelezwa kuwa matumizi ya madawa ya kulevya, imani potofu na malezi duni ni miongoni mwa sababu zinazosababisha kufanyika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana katika jamii.

Akizungumza na Chai FM mara baada ya kufungua kikao cha watetezi wa haki za wanawake na wasichana kilichokutanisha asasi za kiraia wilayani hapa Bw.Teddy Siame ambaye ni afisa maendeleo ya jamii amesema kuwa watoto wakikosa alezi sahihi katika familia huangukia kwenye mikono ya watu waovu hivyo kuwafanyia ukatili.

Siame amesema muendelezo wa utoaji elimu ya mara kwa mara katika jamii inasaidia kupunguza vitendo hivyo.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii Bw. Siame

Awali akifungua mafunzo hayo mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Elimisha Bi. Debora Mwanyanje Amesema moja ya majukumu yao ni kusaidia jitihada za serikali kwa kuongeza uelewa wa jamii dhidi ya vitendo vya ukatili.

Sauti ya mkurugenzi wa Elimisha

Ezron Kyejo, Festina Mwakipunga,Victor Mwaigwisya na Maria Petter ni baadhi ya washiriki katika kikao hicho wametoa rai kwa jamii kushiriki kumlinda mwanamke na msichana dhidi ya vitendo vya ukatili huku wakisisitiza utoaji wa taarifa za vitendo hivyo kwa mamlaka husika.

Sauti za washiriki

Shirika la Elimisha ni shirika lililoanzishwa na baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya mwaka 2009 na kusajiliwa 2010 wakilenga kutoa elimu kwa ukubwa zaidi juu ya vitendo vya ukatili katika jamii.