Chai FM

Serikali yamwaga ajira Rungwe

12 November 2026, 8:15 pm

mkuu wa wilaya ya Rungwe akiongea na vikundi ya vijana [picha na Lennox Mwamakula]

ikiwa vijana wakikabiliana na suala la ajira nchini serikali kupitia wakala wa barababa wilayani Rungwe imetoa mikataba ya ajira kwa vijana

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Wakala wa Barabara za mjini na vijijini [TARURA] mkoa wa Mbeya imeingia mikataba kumi na mbili kwa vikundi kumi na mbili vya kijamii  kwa halmashauri za Runngwe na Busokelo kwa kufanya shughuli za kulinda miundombinu ya barabara.

hafla hiyo imefanyika kijiji cha kalalo kata ya Lufingo na imeongozwa na mkuu wa ilaya ya Rungwe mh, Jaffar hanniu ambaye amewataka vijana hao kufanya kazi iliyo kusudiwa

Akisoma taarifa  mbele ya mkuu wa wilaya ya Rungwe  meneja Tarura wilaya ya Rungwe Derick Kamala amesema kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa mwaka wa fedha 2026/2027 jumla KM79.6 zitatekelezwa kupitia mpango wa CBRM[Community Based RoutineMaintenance] kwa kutumia vikundi vya kijamii

Hata hivyo meneja huyo wa Tarura amesema lengo ya mradi huo kuhakikisha barabara zote ziwe katika hali nzuri na kunzwa kwa kipindi chote cha mwaka pamoja na kuinua kipato kwa vijana na jamii kupitia matengenezo madogo madogo ya Barabara hizo zilizo chini ya Tarura.

sauti ya Meneja Tarura

Akibidhi vifaa pamoja na mikataba ya utekelezaji wa shughuli hiyo Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh, Jaffar Hanniu amesema mpango huo ni muhimu kwani unaenda kuinua uchumi wa vijana pamoja jamii kwa ujumla na kuwataka vijana kufanya kazi kwa uwaminifu

sauti ya mkuu wa wilaya1

Aidha Hanniu amesema kupitia mpango huo wa CBRM amewasisitiza vijana waliopata fursa hiyo kuwa wazalendo na waminifu na wenye kujituma katika kazi zao za kila siku kwa manufaa ya wilaya,mkoa na Taifa kwa ujumla

sauti ya mkuu wa wilaya 2

Kwa upande wao wanufaika wa mradi huo wa CBRM wamesema kutokana vijana kuaminiwa na serikali hiyo wanakwenda kutekeleza yale yote ambayo yanatakiwa kutekelezwa kwa kiwango kinacho hitajika

sauti ya wanufaika

Ikumbukwe kuwa jumla ya shilingi milioni 111,940.00o mradi huo wa Community Based RoutineMaintenance [CBRM] zinakwenda kuwanufaisha vijana hao