Boma Hai FM

HRT SACCOS huduma kwa ajili ya wanachama

9 October 2026, 10:10 am

Pichani ni meneja wa HRT SACCOS Upendo Lyatuu (wa tano kulia)watumishi na baadhi ya wanachama katika kilele cha wiki ya huduma kwa wateja (picha na Calster Marandu)

HRT SACCOS yawataka wanachama kutoa maoni ,ushauri namna chama hicho kinavyofanya kazi zake ili kuongeza ufanisi zaidi.

Na Elizabeth Mafie& Teras Munishi

Wanachama wa  chama cha akiba na mikopo Hai Rural Teachers SACCOS wametakiwa kutumia huduma zinazotolewa na chama hicho pamoja na kutoa maoni kuhusu uendeshaji wake, ili kusaidia kuboresha huduma na kukiendeleza zaidi.

Pichani ni Meneja wa HRT SACCOS Upendo Lyatuu (wakwanza kushoto)pamoja na mwenyekiti mwalimu Alex Warioba katika kilele cha wiki ya huduma kwa wateja(picha na (Calster Marandu)

Kauli hiyo imetolewa na meneja wa SACCOS hiyo Upendo Lyatuu Oktoba 8, 2026 wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja iliyokuwa na kauli mbiu “Huduma kwa ajili ya wanachama”, ambapo viongozi wamesema maoni ya wanachama ni muhimu katika kuwasaidia kutambua changamoto na kuchukua hatua pale panapohitajika.

Sauti ya meneja HRT SACCOS Upendo Lyatuu.

Naye Mwenyekiti wa HRT SACCOS mwalimu Alex Warioba amesema katika wiki  ya huduma kwa wateja,chama hicho kimefanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuwatembelea wanachama waanzilishi na kuwapatia zawadi kama sehemu ya kuwathamini kwa mchango wao katika maendeleo ya chama.

Sauti ya mwenyekiti wa HRT SACCOS Mwalimu Alex Warioba.

Akizungumzia manufaa ya huduma zinazotolewa na HRT SACCOS, mwanachama Gadieli Mmari ambaye amejiunga na chama hicho tangu mwaka 2013, amesema amenufaika na huduma mbalimbali ikiwemo mikopo iliyomsaidia kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya mwanachama Gadiel Mmari.
Pichani ni baadhi ya wanachama wa HRT SACCOS katika kilele cha wiki ya huduma wakipata kifungua kinywa.(picha na Calister Marandu)

Kwa upande wake mwanachama na mtumishi mstaafu Anna Mzuguno  amepongeza HRT SACCOS kwa kutoa huduma bora na kuhakikisha wanachama wanapata mikopo kwa wakati, akisema wiki  ya huduma kwa wateja  imekuwa fursa muhimu ya kuwafanya wanachama wajisikie kuthaminiwa.

Sauti ya mwanachama Anna Mzuguno.