Boma Hai FM

Ulevi chanzo cha uhalifu Machame

7 February 2024, 5:57 pm

Diwani wa Kata ya Machame Magharibi Martini Munisi akiwa katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Nronga (picha na Janeth Joackim)

Kutokana na baadhi ya wananchi kutumia vilevi mbalimbali wakati wa kazi imetajwa kuwa sababu ya vitendo vya uhalifu pamoja na ukatili.

Na Janeth Joackimu

Wananchi wa kijiji cha Nronga Kilichopo kata ya Machame Magharibi wametakiwa kuacha tabia ya unywaji wa pombe uliopitiliza hasa nyakati za kazi kwani pombe inasababisha vijana kutojihusisha katika ufanyaji wa kazi na kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na vitendo visivyo péndeza katika jamii.

Kauli hiyo imetolewa na  Diwani wa Kata ya machame  Magharibi  katika  kikao kilichoandaliwa na Diwani huyo  kwa kushirikiana na wanachi katika Kijiji Cha Nronga kata ya Machame Magharibi.

Munisi amewataka pia wananchi kukemea vitendo vya kikatili kwa watoto na kuwataka kutolea taarifa vitendo vya kikatili katika kituo Cha polisi pindi wanapoona matukio ya kihalifu.

Mmoja wa wananchi wa Kijiji hicho amewahasa wananchi wenzake kuonyesha ushirikiano kwa serikali hususani jeshi la polisi  kipindi anapohitaji kumkamata mwahalifu kwa ajili ya uchuguzi.

Kwa upande wake askari wa kata hiyo Glory John amewataka wananchi kufanya kazi halali kwa kujitafutia kipato kwa njia iliyo halali ili na kuacha kubweteka na kujiingiza katika tamaaa ya kujipatia Kipato kwa njia isiyo halali.

Kwa mujibu wa Glori amewahimiza  wazazi kuacha kupokea zawadi au  fedha kutoka kwa watoto wao bila kufahamu kazi au shughuli anayofanya ya kujipatia kipato.