Boma Hai FM

Kamati ya kudumu ya bunge yaridhishwa na ujenzi wa shule ya sekondari Saashisha

15 March 2024, 7:56 pm

Wananchi wa kata ya Muungano wakimpokea kwa furaha mbunge wao Saashisha Mafuwe ambae pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge Tamisemi (picha na Edwin Lamtey)
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Timisemi katika picha ya pamoja wakiwa katika shule ya sekondari Saashisha ikiwa ni moja ya mradi wa maendeleo walioukagua(picha na Edwin Lamtey)

Kamati ya kudumu ya bunge ya Tamisemi yakagua miradi jimbo la Hai, Saashisha Sekondari yawaridhisha wajumbe wa kamati hiyo.

Na Edwin Lamtey

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa imeeleza kuridhishwa na ujenzi wa shule ya Sekondari Saashisha iliyo jengwa Kata ya Muungano Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza katika ziara hiyo Machi 14.2024, Mwenyekiti wa Kamati ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi Denis Londo amesema kuwa Kamati imeridhishwa na ujenzi wa shule hiyo na kupongeza jitihada zote zolizotumika kufanikisha mradi huo.

“Tumeridhishwa na kazi ya ujenzi wa Shule hii ya Sekondari Saashisha na kamati imekosa maswali ya kuuliza hapa,kazi ni kubwa na ndicho RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan anachokitaka wakati wa kutekeleza miradi” alisema Mwenyekiti Londo.

Aidha ameweka wazi kuwa upatikanaji wa jina la shule “SAASHISHA” umefuata taratibu zote kuanzia kwa wananchi wenyewe hadi Serikali kupitisha jina hilo hivyo hakuna shaka kwa kazi ya Mbunge huyo.

Akizungumza katika ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati hiyo ameishukuru Serikali kwa kukubali kumpatia fedha za kutekeleza mradi huo muhimu ili kuondoa changamoto ya Wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

“Bado kuna ukamilishaji wa ujenzi ikiwemo ujenzi wa jiko,uzio na uwekaji wa samani za ndani,kazi zote hizo zitakamilika na ndio furaha yangu kuona mradi huu unatoa huduma niliyokuwa natamani” alisema Saashisha.

Shule hiyo ya Sekondari Saashisha imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 584 ambapo mpango uliopo ni kuifanya kuwa shule ya bweni kwa kidato cha tano na sita