Boma Hai FM

SHIUMA Hai kufanya maonesho mwenge wa uhuru 2024

7 March 2024, 5:22 pm

Wachama wa chama cha wamachinga wilaya ya (SHIUMA) wakiwasiliza viongozi wao wakati wakitolea ufanunuzi wa maonesho ya mwenge wa uhuru 2024 (picha na Janeth Joachim)

Hai Kuelekea kuashwa kwa mwenge kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 2 April wafanyabiashara wadogowadogo maarufu machinga wilayan Hai wameaanda maonyesho makubwa ya bidhaa mbalimbali za utamaduni sanaa na utalii

Na Janeth Joachim

Kuelekea kuashwa kwa mwenge kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 2 April wafanyabiashara wadogowadogo maarufu machinga wilayan Hai wameaanda maonyesho makubwa ya bidhaa mbalimbali za utamaduni sanaa na utalii yatakayofanyika  katika viwanja vya  shule ya Hai day kuanzia  April  1 hadi  April 4 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na katibu wa shirikisho la wamachinga wilaya ya Hai (SHIUMA) Paul Mwalongo alipozungumza na waandishi wa habari pamoja na wamachinga  katika ukumbi wa Dolfin na kusema lengo la maonyesho hayo ni kutumia fursa waliyopata kutoka serikalini ya mwenge kuwashwa katika mkoa wa Kilimanjaro na kupita katika ukaguzi na  uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha Mwalongo amesema kufika  kwa mwenge katika wilaya ya Hai kutazindua mradi wa SHIUMA wa wilaya ya Hai.

Naye katibu wa SHIUMA mkoa wa Kilimanjaro  Stevin  Kavishe amewataka wananchi na wamachinga  kujitokeza kwa wingi katika kuupokea na kuulaki mwenge wa uhuru 2024.

Kwa upande wa machinga wameleza kuwa wamejipanga kwa kuonyesha bidhaa mbalimbali.

Magila Bakari mmoja wa wamachinga wilayani Hai

Maonyesho  hayo ya SHIUMA yana kauli mbiu ya mbio za  mwenge  wa uhuru isemayo “Tunza Mazingira na shiriki katika uchaguzi wa serikali za mtaa kwa  ujenzi wa Taifa endelevu”.