Boma Hai FM

Wananchi Hai watakiwa kushiriki katika ujenzi wa miradi kuchochea maendeleo

18 April 2026, 3:50 pm

Pichani ni afisa elimu ya watu wazima wilaya ya Hai Emmaculata Mgaza(aliyesimama) diwani kata ya Machame Kaskazini ambae ndie makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Hai Trael Mboya( wa kwanza kulia) pamoja na viongozi wengine wakiwa katika kikao cha kukabidhi mradi(picha na Anasta Urio)

Wananchi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wameaswa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuchangia nguvu kazi na kuilinda, ili kuhakikisha inakamilika kwa ufanisi na kuleta manufaa kwa jamii pamoja na vizazi vijavyo, Serikali imeendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kutoa zaidi ya shilingi milioni 78 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya vyoo katika shule za msingi Mulama na Mkwamatu, huku viongozi wakisisitiza uwajibikaji, uzalendo na matumizi sahihi ya fursa za kiuchumi zinazotokana na miradi hiyo.

Na Anasta Urio

Hai- Kilimanjaro

Wananchi wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kutoa ushirikiano katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ikiwa ni pamoja nakujitolea nguvu kazi ili kufanikisha miradi hiyo kwa ufanisi.

Hayo yamesemwa April 16 , 2026 na afisa elimu ya  watu wazima wilaya  Emaculata  Mgaza wakati akikabidhi miradi ya maendeleo kwa shule ya msingi Mulama  ambapo amekabidhi fedha za ujenzi wa matundu kumi na mbili ya vyoo na shule ya msingi Mkwamatu matundu kumi na mbili ya vyoo yatakayogharimu zaidi ya shilingi milion 78.

Pichani ni wananchi mbalimbali waliojitokeza kwa ajili ya kupokea mradi (picha na Anasta Urio)

Ameeleza kuwa ushirikishwaji wa jamii utaimarisha ulinzi na utunzaji wa miradi Hiyo kwani wananchi wataulinda na kuuthamini kwa kuwa wanatambua umuhimu wake ambapo kutokufanya hivyo fedha hizo zitashindwa kufikia lengo .

Sauti ya afisa elimu ya  watu wazima wilaya  ya Hai Emaculata  Mgaza

Kwa upande wake Diwani  wa kata ya Machame Kaskazini Trael mboya ameishukuru serikali kwa kuleta fedha katika kata hiyo  na kuwataka wananchi wa eneo hilo kutumia fursa hiyo kujinufaisha kiuchumi kwa kuomba nafasi mbalimbali za kazi katika mradi huo.

Sauti ya diwani kata ya Machame Kaskazini na makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Hai Trael Mboya.

Nae  afisa maendeleo ya jamii Tahafifu Shoo ameeleza kuwa wananchi  wanapaswa kuwa mabalozi  wazuri katika kulinda na kutunza  miradi iliyopo kwenye maeneo yao kwani miradi inatekelezwa na serikali kwani lengo ni kunufaisha jamii iliyopo  na vizazi vijavyo.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii Tahififu Shoo

Hata hivyo Mwenyekiti wa kijiji cha mulama Evarest Kweka amesema kuwa yeye yupo tayari kujitolea anapohitajika na amewataka wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha mradi huo kwa wakati jamii zingine nao wapate kupata miradi hiyo.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Mulama Evarest Kweka

Nao wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kupokea mradi huo wameeleza historia ya shule hizo huku wakiishukuru serikali  kwa kukumbuka  shule hizo  huku wakiiomba serikali ikamilishe ujenzi wa Nyumba za walimu Ili kuweka  mazingira Rafiki na salama  ya kazi kwa watumishi .