Boma Hai FM

Makala: Mkenda ahamasisha kilimo cha parachichi Rombo

8 December 2023, 11:40 am

Mbunge wa Rombo Prof Mkenda akikabidhi moja ya miche ya parachichi kwa wananchi jimboni kwake. picha na Elizabeth Mafie

Mbunge wa Jimbo la Rombo Pro Adolf Mkenda amekabidhi Miche ya maparachichi zaidi ya elfu moja kwa wakulima kutoka vijiji mbali mba doli Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Na Elizabeth Mafie

Mbunge wa Jimbo la Rombo Prof Adolf Mkenda amekabidhi Miche ya maparachichi zaidi ya elfu moja kwa wakulima kutoka vijiji mbali mbalimbali Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro lengo ikiwa ni kuwaepushia wananchi hao hali ya utegemezi kwa kuwaongezea vyanzo vya mapato kupitia shughuli za kilimo.

Zoezi hilo limefanyika hii leo katika Kata ya Kirongo Samanga Tarafa ya Useri Parokia ya Mtakatifu Yohanne Mbatizaji Useri Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro

Aidha kila kijiji kimoja kimepatiwa miche 93 ambapo viijiji 16 vimenufaika na miche hiyo ya parachichi huku wakulima hao wakitakiwa kuzingatia elimu ya upandaji wa miche hiyo .

Pro Mkenda amesema miche hiyo ya marachichi haijaja kwa lengo la kukata au kuharibu zao la kahawa na migomba bali kuongeza zao la kilimo cha biashara kwa wananchi ungana nami ninaekuletea makala hii na mwaandaji wako Elizabeth Mafie.

Kusikiliza makala hii bonyeza hapa