Boma Hai FM

Ccm yawaonya wasiofata taratibu

5 February 2024, 12:23 pm

Mbunge wa Rombo ambae ndie Waziri wa Elimu na Teknolojia hapa nchini Profesa Adolf Mkenda akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya miaka 47 tangu kuanzishwa kwa (CCM) kushoto kwake ni mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Suleiman Mfinanga (picha na Janeth Joseph)

Chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro kimewataka baadhi ya wanachama ambao wamekuwa wakikiuka taratibu za chama kwa kuomba kura kwa wananchi kabla ya uchaguzi kuacha mara moja.

Na Elizabeth Mafie

Chama cha Mapinduzi (CCM ) mkoa wa Kilimanjaro kimetoa onyo kali kwa  baadhi ya wanachama ambao wamekuwa wakipita kwa wananchi kuomba kura ikiwa ni katika harakati za kutaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Chama hicho pia  kimewataka wanachama  kuwa watulivu na wenye kufuata taratibu zilizowekwa ili kupata viongozi bora watakao tekeleza ilani ya chama kikamilifu.

Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Suleiman Mfinanga wakati wa maadhimisho ya miaka 47 tangu kuanzishwa kwa CCM yaliyofanyika kimokoa  kata ya Shimbi Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya watu ambao tayari wameanza kupita kwa wananchi wakiomba kura ikiwa ni kinyume na taratibu za chama  ambapo ameonya vikali akiwataka kusubiri hadi muda utakapowadia.

Sauti ya mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Suleiman Mfinanga.

Awali akizungumza na wananchi mbunge wa jimbo la Rombo ambae ndie  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia  nchini Profesa  Adolf Mkenda amesema serikali imeendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kuimarisha upatikanaji huduma za kijamii kama vile huduma za afya, elimu na barabara.

Sauti ya Mbunge wa Rombo Profesa Adolf Mkenda.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Chama hicho kwa Wilaya ya Rombo katibu wa CCM Rombo Mery Sule ameainisha kuwa Chama kimeendelea kusajili na kupokea wanacha wapya huku akiwataka wananchama kujitokeza kugombea katika nafasi za uenyekiti wa vitongoji na vijiji muda utakapofika.

Sauti ya Mery Sule katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Rombo.