Boma Hai FM

Kuelekea miaka 60 ya Muungano ,Masama kusini wapanda miti 1650

24 April 2024, 2:32 pm

Diwani wa kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani(aliyebeba miti) akiwa katika zoezi la kupanda miti katika eneo la Zarau(picha na Janeth Joachim)
Diwani wa kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani akipanda mti eneo la Zarau(picha na Janeth Joachim)

Katika kuelekea miaka 60 ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kata ya Masama Kusini wapanda miti,Diwani asema ni utunzaji wa mazingira.

Na Janeth Joachim

Diwani wa kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani  amewataka wananchi  kuotesha miti katika maeneo yao katika Kuelekea miaka 60 ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  na kwamba kwa kufanya hivyo ni kuendelea kutunza mazingira.

Zoezi  la upandaji wa miti umefanyika katika Kijiji Cha Mkombozi kitongoji Cha Zarau  likiongozwa na Diwan wa kata hiyo.

Aidha  Cedrick amesema tukio hilo limefanyika katika kitongoji hicho kwa kuwa  wananchi hao wanatambua na kufahamu umuhimu wa miti katika maeneo yao na kwamba wanaendelea na zoezi hilo la upandaji wa miti ambapo wanatarajia kupanda miti 2000 na tayari wamepanda miti 1650.

Sambamba na hayo amewataka wananchi hao kuwa walinzi katika miti ambayo wameshaotesha kwa kuwa miti hiyo itabaki Kama alama kwa wananchi pamoja na viongozi

Pia  ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na  Rais  Dkt Samia Suluh Hassan,Mkuu wa wilaya ya Hai ,Amiri Mkalipa pamoja na Baraza la Madiwani.

Sauti ya Diwani wa kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mkombozi Fredrick Lebei amesema kuwa miti hiyo waliomba kutoka halmashauri na wakapatiwa na kwamba wanatakiwa kuotesha katika maeneo ya wazi, maeneo ya serikali pamoja na mashuleni na tayari wameanza utekelezaji wa kupanda miti hiyo huku akisema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na watafatilia kwa  utunzwaji wa miti hiyo.