Boma Hai FM

Halmashauri ya wilaya ya Hai yashika nafasi ya kwanza kimkoa mbio za mwenge wa uhuru 2023

11 December 2023, 11:39 am

Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa akimkabidhi zawadi afisa habari wa halmashauri hiyo Riziki Lesuya ambaye alikuwa katika kamati ya uhamasishaji picha na Anasta Urio.

Halmashauri ya wilaya ya Hai imeshika nafasi ya kwanza kimkoa katika mbio za mwenge wa uhuru 2023.

Na Anasta Urio

Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa amezipongeza kamati mbalimbali zilizohusika katika maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru  2023 kwa jitihada walizofanya na kupelekea Wilaya  hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya wilaya sita na halmashauri saba za  mkoa wa Kilimanjaro.

Ameyasema hayo katika kikao cha tathmini ya mbio za mwenge wa  uhuru 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai  ambapo pia maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru 2024 yameanza kufanyika.

Aidha ametoa vyeti kwa kamati zilizofanya vizuri zaidi nakuwataka kuongeza juhudi zaidi katika utendaji kazi  nakuhamasisha wananchi kushiriki zaidi ili kufanya vizuri zaidi katika mbio za  mwenge wa  uhuru kwa mwaka 2024 .

Pia mkuu wa wilaya amewataka watumishi kufanya kazi kwa ufanisi  ili kupata nafasi ya kupewa fedha kwa ajili yakutekeleza miradi mingine ya maendeleo.

Kwa upande wake  mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai   Dionis Myinga amewashukuru wadau  waliotoa michango mbalimbali katika kufanikisha maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 nakuwataka kuwa na moyo wakujitoa katika shughuli za maendeleo.