Boma Hai FM

Baraza la madiwani wilaya ya Siha lampongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo

22 February 2024, 12:37 pm

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Siha katika picha ya pamoja (picha na Elizabeth Mafie)

Kutokana na jitihada za Mkurugenzi mtendaji pamoja na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya siha za ukosanyaji wa mapato,baraza la madiwani wa halmashauri hiyo latoa pongezi.

Na Elizabeth Mafie

Baraza la madiwani wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro limempongeza  mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt Haji Mnasi pamoja  na watumishi kwa  usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Pongezi hizo zimetolewa na  mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Dunkan Urassa kwa niaba ya madiwani wa Halmashauri hiyo wakati akiwasilisha taarifa yake ya katika  mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani ulioketi katika ukumbi wa mkutano wa halmashauri hiyo katika kipindi Cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Hata hivyo Dankani amesisitiza kuongezwa kwa juhudi kubwa zaidi katika ukusanyaji wa mapato ya halmashauri iili  yasaidie katika kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi na kusema kwamba ni vyema fedha hizo zikatumika kulingana na bajeti inavyoelekeza.

Sauti ya mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Siha Dunkani Urasa.

 Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri hiyo Dkt Haji Mnasi ameelezea mbinu walizofanya katika kuongeza mapato pamoja na mikakati waliyojiwekea kama halmashauri katika kuendelea kuboresha vyanzo vya mapato.

Amesema kuwa  mapato ya ndani wamekusanya kwa  asilimia 84 na matarajio yao ni kuweza kufikisha asilimia mia moja na kwamba anawashukuru  kwa ushirikiano madiwani  wote wa halmashauri hiyo na watendaji  kwa ujumla na wote walioshiriki kwa namna yoyote.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Siha Dkt Haji Mnasi.

 Nae mkuu wa wilaya hiyo Dtk Christopher TImbuka amewakumbusha  wananchi  kushiriki katika mbio za  mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwashwa mkoani Kilimanjaro Aprili 2 2024 katika viwanja vya ushirika Moshi mjini hivyo ni vyema viongozi kuhamasisha wananchi ili waweze kushiriki kwa wingi hata utakapo wasili katika wilaya ya Siha.

Hata hivyo baraza Hilo limeketi kwa lengo la kupitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa halmashauri ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo, taarifa za mapato na matumizi, na taarifa ya utekelezaji kutoka kata zote 17 za wilaya hiyo.