Boma Hai FM

Profesa Mkenda akutana na warombo waishio Dar es salaam,wajadili maendeleo.

7 May 2024, 12:10 am

Mbunge wa Rombo na waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia hapa nchini Profesa Adolf Mkenda akizungumza na wananchi wa Rombo wanaoishi Dar es saalam(picha na Elizabeth Mafie)
Mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mangwala akizungumza na wananchi wa Rombo wanaoishi Dar es salaam(picha na Elizabeth Mafie)
Diwani wa kata ya Katangara Mrere Venance Mallel aliyevaa shati la mistari,pamoja na wananchi wa Rombo wanaoishi Dar es Salaam wakiwa katika mkutano(picha na Elizabeth Mafie)
Wananchi wa Rombo wanaoishi Dar es salaam wakiwa katika mkutano(picha na Elizabeth Mafie)

Wanananchi kutoka Rombo Mkoani Kilimanjaro waishio Dar es saalam wakutanishwa na Mbunge wao na kujadili kuhusu maendeleo ya Rombo na namna ya kutatua changamoto mbalimbali.

Na Elizabeth Mafie

Mbunge wa Rombo Profesa Adolf Mkenda ambae pia ni waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia hapa nchini amefanya mkutano na wananchi wa Rombo waishio Dar es Salaam lengo ikiwa ni kujadiliana Kwa pamoja kuhusiana na maendeleo yaliyofanyika Rombo na yanayoendelea kufanyika pamoja nakuzitolea ufafanuzi Kero watakazoziibua.

Mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Rombo wanaoishi Dar es Salaam,baadhi ya wabunge wa mkoa wa Kilimanjaro na madiwani kutoka Kata 28 za Halmashauri ya Rombo pamoja na Mkuu wa  wilaya hiyo umefanyika katika ukumbi wa Cadnal Adam uliopo Msimbazi Center jijini Dar es saalam.

Profesa Adolf  Mkenda amesema kuwa amekuwa na utararibu wa kuelezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika Rombo ikiwemo miradi ya barabara,Afya,maji,na Elimu  na kwamba sio Mara ya kwanza kufanya hivyo bali ni muendelezo na atakuwa anafanya hivyo ili wananchi wote waelewe maendeleo ya Rombo.

“Utaratibu huu tumeanza sio Jana ,sio juzi Ni tangu zamani tulianza Arusha, Dodoma na Leo tuko Dar es Salaam, lengo Letu hapa Ni kueleza namna tunawajibika, tunafanya sana mikutano Rombo, juzi hapa tumefanya mkutano tarafa ya Mwengwe viongozi wote  tumekutana,  na tulikuwa na power point kuelezea nini kimefanyika Kila Kata na takatoka tukaenda kwenye mkutano wa hadhara Kingachi, Kwa hiyo hatuji hapa kanakwamba ni Mara ya kwanza,haya mambo tunayafanya kule”Amesema Mkenda.

Sauti ya Mbunge wa Rombo na waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia hapa nchini Profesa Adolf Mkenda.

Kwa upande wake mwananchi wa Rombo anayeishi Dar es Salaam  Felisian Mtenga amesema kuwa wamefurahishwa na Jambo hilo la kukutana Kwa pamoja na kujadiliana kuhusu maendeleo  ya Rombo na kwamba wangependelea kuanzishwa Kwa Benk ya Rombo kwani wanapokuwa na benki  yao ni rahisi kufanikiwa lazima kuwa na benki ,pamoja na kupata mtaji wa  kuanzisha viwanda na kuwa na uchumi endelevu.

Sauti ya mwananchi wa Rombo anayeishi Dar es saalam Felisian Mtenga.

Nae Mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mangwala amesema kuwa wilaya ya Rombo wameenda kutekeleza miradi mingi ya maendeleo,Kwa kupata fedha kutoka serekali kuu na kwamba wamepokea shillingi bilioni 12 Kwa ajili ya miondombinu pekee,hivyo Kazi inaendelea Rombo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mangwala.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amempongeza Mbunge wa Rombo Profesa Adolf Mkenda na kwamba wananchi wa Rombo wamepata Mbunge anaefanya Kazi nzuri hivyo wamuunge mkono ili aweze kuhitimisha Kazi hiyo.

Sauti ya Mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe.