Boma Hai FM
Boma Hai FM
18 April 2026, 4:24 pm

Madereva wametakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa kuepuka ulevi, matumizi ya simu wanapoendesha, pamoja na kufanya maamuzi sahihi wanapokutana na changamoto barabarani, ili kupunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wote wa barabara.
Na Oliva Joel
Hai- Kilimanjaro
Katika kuepuka ajali za barabarani hasa katika kipindi cha mvua,madereva wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuchukua tahadhari mbalimbali ili kujilinda na kuwalinda watumiaji wengine wa barabara.
Hayo yamebainishwa Aprili 17 2026 na Sajent Ramadhan Juma kutoka kituo cha polisi Bomang’ombe kitengo cha usalama barabarani alipokuwa akizumgumza katikia kipindi cha Siku mpya kinachorushwa na Redio Boma Hai Fm.
Sajent Rama amezitaja tahadhari ambazo madereva wanapaswa kuchukua ikiwa ni pamoja na kuepuka mwendo kasi,kufuata alama za barabarani,kuepuka kuyapita magari bila tahadhari pamoja na kuepuka ulevi.
Akizungumzia suala la ulevi uliopindukia kwa baadhi ya madereva wa magari binafsi,amewataka madereva kutoendesha magari yao pindi wanapokuwa wamelewa badala yake waombe usaidizi wa polisi ili kuhakikisha wanakuwa salama kwani jeshi la polisi lina jukumu la kulinda raia na mali zao.
Sajent Ramadhani amekemea tabia ya baadhi ya madereva wanaotumia simu wakati wa kuendesha gari na kusema kuwa hali hiyo inaondoa umakini barabarani na kusababisha ajali.
Hata hivyo amewataka madereva kutotumia simu wanapokuwa barabarani ili kuwalinda wao na watiaji wengine wa barabara.