Boma Hai FM

Bodi ya maji Uroki Bomang’ombe yafanya uchaguzi, mwenyekiti aahidi ushirikiano

8 August 2024, 12:45 pm

Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiri Mkalipa ambae alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi wa bodi ya maji Uroki Bomang’ombe akizungumza na wajumbe( picha na Jonhson Nkya)

Bodi ya maji Uroki Bomang’ombe yafanya uchaguzi wa mwenyekiti,makamu mwenyekiti,pamoja na wajumbe wawili wa bodi hiyo ambao wataongoza kwa miaka mitatu,wahaidi ushirikiano na mifumo mipya ya kurahisisha huduma kwa wateja.

Na Johnson Nkya

Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa ametoa wito kwa wananchi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kutunza miundombinu ya maji iliyopo ili kurahisisha utaoji wa huduma bila kikwazo na kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hiyo.

Mkalipa amesema hayo katika uchaguzi wa bodi ya maji Uroki bomangombe ambapo bodi hiyo imefanya uchaguzi wa mwenyekiti, makamu mwenyekiti pamoja na wajumbe katika ofisi kuu zilizopo kata ya Romu August 7, 2024. 

Aidha ametoa pongezi kwa bodi iliyomaliza muda wake kwa kufanya kazi  nzuri kwa kipindi chote walichowahudumia wananchi nakuitaka bodi iliyoingia madarakani kufanya kazi kwa bidii na uwaminifu na kutoa ushirikiano ili  kuweza kutatua changamoto zitakazotokea katika bodi na wananchi kwa ujumla.

Wajumbe wakiendelea na zoezi la kupiga kura(picha na Johnson Nkya)

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo Batista Ngulu  aliyechaguliwa kwa kura 91 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 47 amesema kuwa atatoa ushirikiano kwa ujumbe ngazi ya kata na vijiji 11 vya bomangombe  ili kutatua changamoto za upatikanaji wa maji na kwamba watumiaji wa mradi huo wanatakiwa kulipa ankara za maji kwa wakati na kwa usahihi ili kuondoa usumbufu wa malimbikizo ya bili na kuwaomba wananchi kutunza mazingira ili kuendelea kulinda vyanzo vya maji.

Sauti ya mwenyekiti aliyechaguliwa Batista Ngulu

Miongoni wa wajumbe walioshiriki katika uchaguzi wa bodi hiyo wamesema kuwa wamefurahishwa na uchaguzi na kwamba wa na imani na viongozi hao kwani wateendelea kuwa kielelezo kizuri kwa kuhukikisha kuwa huduma inapatikana.

Wajumbe wakimsikiliza mgeni rasmi(picha na Johnson Nkya)

Naye meneja wa Ruwasa wilaya ya Hai Imanuel Mwampashi  amesema kwamba sheria ya maji namba tano ya mwaka 2019 kifungu cha 34 (1) kwamba uchaguzi unatakiwa ufanyike kila baada ya miaka mitatu  na kwamba viongozi waliochaguliwa wataongoza bodi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu pia  bodi hiyo inatengemea kuendelea kutoa huduma ya maji kwa asilimia mia moja kwa  wananchi  wake na kuendelea kuboresha kwa kutumia mita za maji za kisasa ambapo mteja atakuwa akitumia mita za malipo ya kabla(Pre paid metre).

Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Batista Ngulu akitoa shukrani kwa wajumbe waliomchagua(Picha na Johnson Nkya)

“Tunategemea kutoa maji kwa silimia 100 kwenye maeneo tunatoa huduma ikiwemo vijiji 11 na kata 3 za bomangombe na pia tunataka hii bodi iweze kuhakikisha kuwa wateja wote wanatumia mita za malipo ya kabla­ ( pre paid meter)Amesema Mwampashi.

Sauti ya meneja wa Ruwasa wilaya ya Hai Immanuel Mwampashi