Boma Hai FM

Maafisa ugani Hai wakabidhiwa pikipiki

20 December 2023, 10:03 pm

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai wa pili kushoto akikabidhi pikipiki kwa maafisa ugani (picha na Latifa Botto)

Pikipiki sita zimekabidhiwa kwa maafisa ugani kutoka kata mbalimbali wilayani Hai lengo ikiwa ni kuwafikia wananchi kwa urahisi.

Na Latifa Botto

Wito umetolewa kwa maafisa ugani wote kuzingatia sheria za usalama barabarani pamoja na kupata mafunzo yanayostahili kuhusiana na utumiaji wa vyombo vya moto Kama pikipiki na kutumia vyombo hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa yakuwafikia wananchi.

 Hayo yamesemwa hii Leo na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka wakati akikabidhi pikipiki sita kwa maafisa ugani kutoka kata tofauti  za wilaya ya  Hai ambapo makabidhiano hayo yamefanyika  katika eneo la halmashauri ya wilaya ya Hai.

Amesema kutokana na umuhimu uliopo wa kutii sheria za barabarani pasipo shuruti kwa watumiaji wa barabara ni vema kwa maafisa ugani kujifunza namna ya kuendesha pikipiki ili awapo barabara asipate changamoto yoyote pamoja na hilo pia kuzingatia malengo yaliyokusudiwa kwa kutumia vyombo hivyo vya moto kwaajili ya kuwafikia wananchi kwa kuwahudumia kutokana na changamoto zinazowakumba katika maeneo husika.

Sauti ya mwenyekiti wa Halmashauri Edmund Rutaraka.

Kwa upande wake kaimu wa idara ya mifugo,kilimo na uvuvi ndugu Fraiten Mtika amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia suluhu Hassan kwa kuwaletea pikipiki hizo mpya ambazo ni vitendea kazi muhimu kwaajili ya kuwafikia wananchi na wahitaji popote walipo katika kata zao.

Sauti ya kaimu idara ya mifugo,kilimo na uvuvi Fraiten Mtika.

Nae afisa mifugo,kilimo,na uvuvi Orestesi Rugarabam ametoa shukurani kwa viongozi mbalimbali walioonyesha jitihada za upatikanaji wa pikipiki hizo ambazo zitarahisisha kumtembelea mkulima mmoja mmoja pamoja na kuwahi na kuwahi maeneo ya kazi kwa wakati.