Boma Hai FM

Tyc yaendeleza mafunzo kwa vijana Kilimanjaro

8 December 2023, 8:43 am

Vijana ambao ni wanufaika wa mradi wa boresha maisha kwa vijana wakiwa katika mafunzo.

Vijana zaidi ya ishirini katika mkoa wa Kilimanjaro wamepatiwa mafunzo na shirika lisilo la serekali lijulikanalo kama Tanzania Youth Coalition linalotekeleza mradi wa boresha maisha kwa vijana.

Na Elizabeth Mafie

Vijana kutoka katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali katika mkoa wa kilimanjaro wameendelea kupewa mafunzo na shirika lisilo la kiserekali Tanzania Youth coalition kwa lengo la kuwajenga uwezo katika shughuli wanazozifanya.
Mafunzo hayo yamefayika katika chuo cha ushirika moshi yakihusisha vijana wapatao ishirini ikiwa ni muendelezo wa mradi wa boresha maisha kwa vijana unaosimamiwa na shirika hilo kwa kushirikiana na we effect.
Akizungumza katika mafunzo hayo afisa mradi Josephina Onesmo amesema kuwa mafunzo hayo ni endelevu kwa vijana wanaojihusisha na kilimo pamoja na ujasiriamali ili vikundi vya vijana hao viweze kufikia malengo waliyokubaliana.

CAST JOSEPHINA ONESMO.

Amesema kuwa wanawajengea uwezo vijana walio katika vikundi kwa kuwa wanaamini kuwa vijana wakiwa pamoja na wakaunganisha nguvu inakuwa ni rahisi katika kufikia malengo yao tofauti na kijana akiwa mmoja.

CAST JOSEPHINA ONESMO

Kwa upande wake mnufaika wa mafunzo hayo Godfrey Masawe amesema kuwa mafunzo hayo ni awamu ya tano na kwamba amenuafaika kupitia mradi huo wa boresha maisha kwa vijana na kwamba zipo mada mbalimbali wanazofundishwa ikiwemo usawa wa jinsia na ukatili.

CAST GODFREY MASAWE