Boma Hai FM

Prof Mkenda ahimiza kilimo cha parachichi Rombo

8 December 2023, 4:43 pm

Mbunge wa Rombo Prof Mkenda akikabidhi miche ya parachichi kwa wananchi wa jimbo la Rombo. picha na Elizabeth Mafie

Wananchi wa Rombo mkoani Kilimanjaro wamepatiwa miche ya parachichi zaidi ya elfu moja kwa ajili ya kilimo cha kisasa.

Na Elizabeth Mafie

Mbunge wa Jimbo la Rombo Pro Adolf Mkenda amekabidhi Miche ya maparachichi zaidi ya alfu moja kwa wakulima kutoka vijiji mbali mbali Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro lengo ikiwa ni kuwaepushia wananchi hao hali ya utegemezi kwa kuwaongezea vyanzo vya mapato kupitia shughuli za kilimo.

Zoezi hilo limefanyika hii leo katika Kata ya Kirongo Samanga Tarafa ya Useri Parokia ya Mtakatifu Yohanne Mbatizaji Useri Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro

Aidha kila kijiji kimoja kimepatiwa miche 93 ambapo viijiji 16 vimenufaika na miche hiyo ya parachichi huku wakulima hao wakitakiwa kuzingatia elimu ya upandaji wa miche hiyo .

Pro Mkenda amesema miche hiyo ya marachichi haijaja kwa lengo la kukata au kuharibu zao la kahawa na migomba bali kuongeza zao la kilimo cha biashara kwa wananchi .

Mbunge wa Rombo akizungumza na wananchi kuhusiana na miche ya maparachichi.

Baadhi ya wakulima ambao pia ni wanufaika wa miche hiyo wameeleza changamoto wanazo kutana nazo kwenye kilimo na kuomba kupatiwa msaada wa dawa za kuulia wadudu nyemelezi.

Mmoja wa wanufaika akizungumza mara baada ya kukabidhiwa miche hiyo.