Boma Hai FM

Wananchi Hai watakiwa kutunza mazingira

18 January 2024, 12:16 pm

Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro Amir Mkalipa ( aliyevaa shati nyeupe mbele akiwa na wadau wa mazingira wakielekea kupanda miti katika chanzo cha maji nguni kilichopo kata ya Masama Kati(picha na Elizabeth Mafie)

Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa awataka wananchi kutunza mazingira.

Na Elizabeth Mafie

Wananchi   wilayani  Hai mkoani  Kilimanjaro   wametakiwa kulinda na kutunza mazingira  ili kuhifadhi vyanzo vya maji dhidi ya uharibifu na kubaki salama kwaajili ya vizazi vijavyo.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa katika zoezi la kupanda miti katika chanzo cha maji kilichopo  katika kijiji cha Nguni kata ya Masama Kati,ambapo amesema kuwa watakao bainika wamefanya uharibu wa chanzo cha maji kwa namna yoyote ile hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na atawajibika kulipa faini nakupanda miti katika eneo hilo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa.

Aidha  wakala wa huduma  za misitu TFS  wilaya ya Hai  Marisia  Alois ameeleza kuwa wamejipanga vyema katika kudhibiti uharibifu wa mazingira hususani  ukatakaji miti ovyo na kulima kwenye vyanzo vya maji kwani wanavyombo imara vya kudhibiti uharibifu huo.

Sauti ya wakala wa huduma za misitu (TFS) wilaya ya Hai Marisia Alois

Kwa upande wake afisa mazingira kutoka bodi ya maji bonde la Pangani Brown Mwangoka  akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Bonde la Pangani  amesema kuwa wameweka mabango matatu kwenye mipaka ya vyanzo vya maji yakuonyesha katazo la kufanya shughuli za kibinadamu katika chanzo cha maji ikiwa ni pamoja na  kupanda miti zaidi ya mia tano katika chanzo hicho

Kwa mujibu wa , Brown ameishukuru serikali ,taasisi na wadau mbalimbali kwa kuendelea kutoa ushirikiano wao katika jitiada zakuhakikisha ulinzi na utunzaji wa vyanzo vya maji unazingatiwa katika kupambana na changamoto wanazokumbana nazo kama kilimo, na ujenzi katika  vyanzo vya maji.

Sauti ya afisa mazingira kutoka bodi ya maji Bonde la Pangani Brown Mwangoka