Boma Hai FM

‘Maendeleo ya kijiji yanaletwa na wananchi wenyewe’ – Edwine Lamtey

2 February 2026, 4:58 pm

Pichani ni Afisa mtendaji wa Kijiji cha Kwasadala Edwine Lamtey ( aliyesimama) pamoja na wajumbe wa kamati ya kijiji (Picha na Henry keto)

Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro

Wananchi wa kijiji cha kwasadala kata ya Masama Kusini, Wilaya ya Hai Mkoani Kilimajaro wamejitokeza kwa wingi kusikiliza bajeti ya mapato na matumizi ya kijiji pamoja na kujadili maendeleo ya kijiji chao.

Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro

Wananchi wa Kijiji cha Kwasadala Kata ya Masama kusini, wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro wamehimizwa kujitokeza katika shughuli za maendeleo katika kijiji chao pamoja na kuwa walinzi wa mali za Umma ikiwa ni pamoja na ulinzi wa miradi ya maendeleo katika kijiji na maeneo wanayoishi.

Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha Kwasadala Edwaine Lamtey wakati wa mkutano wa kijiji uliofanyika tarehe 28, Januari 2026 katika kijiji cha kwasadala, ambapo amesoma bajeti ya mapato na matumizi ya kijiji ambayo wananchi wameipokea na kuunga mkono juhudi za serikali yao kuleta maendeleo katika kijiji chao.
Mkutano huo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwasadala Ndugu Yasin Kweka kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kijiji, Edwine Lamtey, ambapo amewasilisha taarifa ya kina ya mapato na matumizi kwa kipindi husika.

Sauti ya Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kwasadala Ndugu Edwine Lamtey akizungumza baada ya mkutano wa kijiji cha Kwasadala
Pichani ni wanakijiji cha Kwasadala waliojitokeza kwenye kikao cha kijiji kilichojadili masuala mbalimbali yakimaendeleo katika kijiji chao (Picha na Henry Keto)

Katika mkutano huo, viongozi wa kijiji wameeleza kuwa Kijiji cha Kwasadala kimeelekeza nguvu kubwa katika ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya kijiji, ambapo kwa sasa ujenzi huo umefikia hatua ya kupaua, Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wameombwa kuendelea kujitolea kwa hali na mali ili kukamilisha ujenzi wa jengo hilo, ambalo linatarajiwa kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wa kijiji hicho.

Sauti za Wajumbe wa kamati ya serikali ya kijiji wakizungumzia maendeleo ya kijiji chao.

Nao wananchi wa Kijiji cha Kwasadala wameishukuru serikali ya kijiji kwa jitahada kubwa za ujenzi wa Ofisi ya kijiji ambayo itarahisisha utoaji wa huduma kwa Wananchi, wameahidi kujitolea kwa moyo mmoja kuleta maendeleo kwa manufaa ya wananchi wote.