Boma Hai FM

Mfumo wa kubaini ukame tumaini jipya kwa wakulima Kilimanjaro

13 April 2024, 8:58 am

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hai mwalimu Hussein Kitingi ambae alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho akizungumza na wadau wa maji pamoja na wakulima(picha na Elizabeth Mafie)
Wadau wa maji pamoja na wakulima wakiwa katika kikao(picha na Elizabeth Mafie)

Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa yakileta athari kwa wakulima na watumia maji Taasisi ya Nelson Mandela ya sayansi na teknolojia wabaini mfumo wa kubaini ukame mapema.

Na Elizabeth Mafie

Wadau wa Mazingira kutoka taasisi ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia mkoani Arusha wameanzisha mfumo mpya wa kuweza kubaini mapema athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo hupelekea ukame na kusababisha athari kwa wakulima.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa maji, pamoja na wakulima kilichofanyika leo,Aprili 12 2024 katika ukumbi wa Idara ya Maji wilayani Hai Dk. Ana Msigwa kutoka taasisi ya Nelson Mandela amesema kuwa wameamua kufanya utafiti huo wa kugundua mfumo wa mapema wa  ukame ilikumsaidia mkulima wakiti mzuri wakuanza kulima.

 Amesema mfumo huo utasaidia pia kutambua ukame atika Bonde la Pangani ambapo waliwasilisha kwa wadau hao ili kuepukana na  mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa na athari Kubwa hasa kwa wakulima.

 ” wakulima wengi ni wahanga wabadiliko ya tabia nchi kutokana na kutotambua wakati upi walime na upi wasilime na kwamba mpaka sasa tayari wameweka vifaa viwili, kimoja katika wilaya ya Hai na wilaya ya Siha zilipo mkoani Kilimanjaro.” Ameeleza Dk Anna

Dk. Anna amesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia katika kupata takwimu za hali ya hewa ,hasa wakati wa mvua na kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi wakulima wamekuwa wakipata athari katika mazao yao ,hivyo mfumo huo utawasaidia kutabiri mapema kuwa walime kutokana na utabiri huo.

Sauti ya Dr Anna Msigwa Mhadhiri kutoka Taasisi ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia Arusha.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Bodi ya maji Bonde la Pangani Kanda ya Kaskazin Patris Otieno ameishukuri Taasisi hiyo ya Nelson Mandela kwa kuleta mradi wa utabiri wa Hali ya hewa kwani  utawasaidia Bonde la Pangani kwakuwa itaongeza wigo kwa wakulima pamoja na watumia maji kuweza kufahamu changamoto ambazo zinapelekea ukame na kuwa na taarifa mapema ili kuweza kuepuka athari zinazoweza kutokea.

Sauti ya Patrisi Otieno kaimu mkurugenzi Bonde la Pangani kanda ya Kaskazini.

Nae Kaimu Mkurugenzi wilaya ya Hai ambae alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho Hussein Katingi amesema kuwa mradi huo utawanufaisha watumia maji pamoja na wakulima kwani suluhisho la changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi tayari imepatikana na kwamba rasilimali maji itumike kwa uendelevu.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wilaya ya Hai ambae ndie mgeni rasmi Mwalimu Hussein Kitingi.

Mmoja wa wadau wa maji ambae ni mwenyekiti wa watumia maji mto Kware Wilfred Massawe amesema kuwa mradi huo utawasaidia wananchi kwa ujumla kutambua ni wakati gani wa kufanya shughuli za kilimo ,pamoja na kujua  wapande mazao ya aina gani shambani katika msimu huo.

Sauti ya mwenyekiti wa watumia maji mto Kware Wilfred Massawe.