Boma Hai FM

Soko la Mbuyuni lateketea kwa moto

6 February 2024, 8:26 am

Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdini Babu alipofika soko la mbuyuni lililoteketea kwa moto leo usiku(picha na Devis Minja)

Soko la Mbuyuni limeteketea kwa moto na kuwasababisha hasara kwa wafanyabiashara wa soko hilo huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani.

Na Elizabeth Mafie

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amefika soko la Mbuyuni lililoteketea kwa moto usiku huu na kutoa pole na  maagizo .

Akiambatana na kamati ya ulinzi Wilaya na Mkoa RC Babu amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya uchunguzi vinachunguza tukio hilo la moto.

Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa hakuna kilicho bakia na kwamba anawapa pole wafanyabiashara na kuwataka  wawe  watulivu wakati tukio hilo likichunguzwa  ili kubaini chanzo cha moto huo.

 Aidha amekemea tabia ya baadhi ya watu kutumia matukio kama hayo kufanya uporaji kwani  haipendizi na badala yake wajikite katika kutoa msaada zaidi.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu.

Nao wafanyabiashara wa soko hilo wamesema kuwa wamepata hasara kwani moto huo umeteketeza mali zao na kwamba wanaiomba serikali kushughulikia swala hilo.

Sauti za wafanyabiashara katika soko la Mbuyuni.

Moto huo ulianza soko la Mbuyuni katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro majira ya saa saba usiku ambapo chanzo cha cha moto huo bado hakijajulikana.