Boma Hai FM

Mbunge Saashisha atoboa siri ya miradi mikubwa Inayokuja Hai

25 July 2026, 8:31 am

Pichani ni mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe( aliyevaa miwani)pamoja na mtangazji wa radio Boma Hai Fm James Gasindi katika kipindi maalum( picha na Oliva Joel)

Mbali na kueleza mafanikio ya miradi ya maendeleo, Mbunge Saashisha amesisitiza umuhimu wa kulinda maeneo ya kimkakati na kuhakikisha changamoto za maji zinapatiwa ufumbuzi.

Na Oliver Joel

Hai – Kilimanjaro

Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Saashisha Mafuwe, amewataka wananchi wilayani Hai  kutumia kikamilifu fursa zinazotokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuboresha maisha yao.

Pichani ni Mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe akiwa katika studio za radio Boma Hai Fm katika mahojihano maalum( picha na Oliva Joel)

Akizungumza Julai 24, 2026 katika kipindi maalum kupitia Redio Boma Hai FM, Saahisha amesema miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa ufugaji wa kisasa unaofadhiliwa na washirika kutoka Uholanzi, unaolenga kuwahamasisha wafugaji kutumia mbinu za kisasa ili kuongeza tija na kipato.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe.

Aidha amesema miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kutekelezwa wilayani Hai, huku akiwasihi wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara ya Bomang’ombe–TPC kutouza maeneo yao kwa kuwa ni eneo la kimkakati linalotarajiwa kunufaika na uwekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe

Kuhusu huduma ya maji  Saashisha  amesema serikali imeendelea kuwekeza katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji, ikiwemo mradi wa shilingi bilioni 3.39 ambao umekamilika pamoja na mradi wa shilingi milioni 900 uliotekelezwa eneo la Kwasadala kwa lengo la kupunguza adha ya upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Akijibu swali la msikilizaji aliyepiga simu kuhusu ukosefu wa maji katika Shule ya Msingi Kingereka, Saashisha  amemuagiza Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Hai kushughulikia changamoto hiyo ili wanafunzi pamoja na wananchi wanaozunguka shule hiyo waweze kupata huduma ya maji safi na salama.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe