Boma Hai FM

HRT Saccos yapaa yaongeza wanachama 659, mali zafikia Bilioni 21

8 September 2026, 3:16 pm

Pichani ni Viongozi wa Chama Cha Akiba na mikopo HRT Saccos (Picha na Henry Keto)

Chama cha akiba na Mikopo HRT Saccos kimeendelea kupata mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya wananchama 659 na kufanya wanachama kufikia 3,323, huku mali za chama zikifikia bilioni 21 mwaka 2025 kutoka bilion 18 mwaka 2024

Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro

Chama cha Hai Rural Teachers SACCOS (HRT SACCOS) kimeendelea kufanya vizuri katika mwaka kwa 2025/2026, baada ya kuongeza idadi ya Wanachama wapya takribani 659 na kufanya idadi ya Wanachama wapatao 3,323. Pia kimeongeza thamani ya mali zake kutoka Shilingi bilioni 18 mwaka 2024 hadi kufikia takribani Shilingi bilioni 21 mwaka 2025.

Hayo yamesemwa na Meneja wa HRT SACCOS, Upendo Lyatu, Septemba 7, 2026, wakati wa mkutano wa dondoo na wanachama wa Tarafa ya Masama, uliolenga kuwapa wanachama taarifa kuhusu mwenendo, mafanikio na maendeleo ya chama.

‎Upendo amewahamasisha walimu na watu wengine ambao bado hawajajiunga na chama hicho kufanya hivyo, akisema wanachama wana fursa ya kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo hisa, akiba, mikopo ya maendeleo, amana za watoto, pamoja na huduma nyingine zenye masharti nafuu.

Sauti ya Manager wa Chama cha akiba na Mikopo HRT Saccos Upendo Lyatuu

Aidha, amewahamasisha walimu na watu wengine ambao bado hawajajiunga na chama hicho kufanya hivyo, akisema wanachama wana fursa ya kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo hisa, akiba, mikopo ya maendeleo, amana za watoto, salary advance pamoja na huduma nyingine zenye masharti nafuu.

Awali Mwenyekiti wa HRT SACCOS, Mwalimu Alex Warioba, wakati akifungua mkutano huo, amewataka wanachama kuendelea kuhubiri na kulinda amani na utulivu wa Tanzania, akisisitiza kuwa mazingira ya amani ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya taasisi na vyama vya ushirika.

‎Mwalimu Warioba amesema HRT SACCOS imeendelea kuwa imara kwa kipindi cha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, huku akitoa wito kwa wanachama kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa viongozi watakaopewa dhamana ya kuongoza chama kwa kipindi kijacho.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo HRT Saccos Mwalimu Alex Warioba
Pichani ni wanachama wa Chama Cha akiba na mikopo HRT Saccos (Picha na Henry Keto)

‎Naye mwanachama wa HRT SACCOS, Honest Assey, ameishukuru SACCOS hiyo kwa kutoa semina ya dondoo, akisema imewasaidia wanachama kufahamu zaidi malengo ya chama, idadi ya wanachama pamoja na sifa na taratibu za mtu anayehitaji kujiunga.

‎Huku akitoa wito kwa walimu na wananchi wengine kujiunga na HRT SACCOS, akisema chama hicho kinaweza kuwa chombo muhimu cha kuwawezesha wanachama kujenga akiba, kupata mikopo na kukuza maendeleo yao kiuchumi.

Sauti ya mwanachama wa HRT SACCOS, Honest Assey

Ametoa wito kwa walimu na wananchi wengine kujiunga na HRT SACCOS, akisema chama hicho kinaweza kuwa chombo muhimu cha kuwawezesha wanachama kujenga akiba, kupata mikopo na kukuza maendeleo yao kiuchumi.

HRT SACCOS inaendelea kuhamasisha wanachama wake kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama, huku ikilenga kuendelea kukua na kuboresha huduma kwa wanachama wake.