Boma Hai FM

Elimu ya watu wazima yatajwa kuwa nyenzo ya kujikwamua kiuchumi

4 September 2026, 7:00 pm

Pichani ni katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Yusuph Nzowa (wa pili kushoto) mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Omary Bomboko (watatu kushoto)mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mangwala (wa kwanza kulia) pamoja na mkuu wa wilaya ya Moshi Godfrey Mnzava wakiwa katika maadhimisho ya kilele juma la elimu ya watu wazima (picha na Oliva Joel)

Jamii imetakiwa kuongeza ushirikiano na wadau wa elimu ili kuwafikia watu wazima ambao hawakupata fursa ya kusoma katika mfumo rasmi, huku elimu hiyo ikilenga kuwajengea ujuzi na maarifa ya kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao

Na Vaileth Silvester

Hai – Kilimanjaro

Jamii imetakiwa kushirikiana na wadau mbali mbali katika sekta ya elimu ili kuwezesha watu  wazima waliokosa elimu katika mfumo rasmi waweze kunufaika na elimu ya watu wazima.

Pichani ni baadhi ya maafisa elimu walioshiriki katika maadhimisho ya kilele cha elimu ya watu wazima(picha na Oliva Joel)

Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Yusuph Nzowa amebainisha hayo Septemba 4,2026  katika maadhimisho ya kilele cha juma la elimu ya watu wazima kimkoa yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kibaoni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Sauti ya katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Yusuph Nzowa

Nae Afisa elimu ya watu wazima mkoa wa Kilimanjaro Jacksoni Mtenga  amesema pamoja na majukumu mengine, lengo kuu ni kuwawezesha wanufaika kupata elimu, ujuzi na kujikwamua kiuchumi

Sauti ya afisa elimu ya watu wazima mkoa wa Kilimanjaro Jackson Mtenga.

Baadhi ya wanufaika wa elimu ya watu wazima akiwemo Bi Christina Lolo  na Bwana Hamisi Moka wameishukuru serikali kwa kuwawezesha kupata elimu ya kusoma, kuandika na kuhesabu kwani imewawezesha kuwa na uelewa wa mambo mbali mbali ikiwemo matumizi ya simu na maelekezo ya dawa.

Sauti ya wanafaika wa elimu ya watu wazima.

Maadhimisho hayo yaliambatana na kutoa hati za pongezi kwa halmashauri na shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita.

Pichani ni baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kilele elimu ya watu wazima(picha na Oliva Joel)

Kaulimbiu ya maadhimisho ya kilele Cha juma la elimu ya watu wazima ni ” Kisomo kwa manufaa ya watu na ustawi wa jamii.”

Pichani ni baadhi ya wanufaika wa elimu ya watu wazima(picha na Oliva Joel)