Boma Hai FM
Boma Hai FM
23 June 2026, 1:32 pm

Serikali imesema itachukua hatua za kuvunja mkataba kati ya Chama cha Ushirika cha Mrososangi na mwekezaji husika endapo ujenzi wa kiwanda cha kuchakata parachichi hautatekelezwa kwa mujibu wa makubaliano yaliyowekwa.
Na Mwandishi wetu
Dodoma
Serikali imesema itavunja mkataba kati ya Chama cha Ushirika cha Mrososangi na mwekezaji husika iwapo mwekezaji huyo atashindwa kutekeleza wajibu wake wa kujenga kiwanda cha kuchakata parachichi kama ilivyoainishwa katika mkataba.
Kauli hiyo imetolewa Juni 22, 2026 na Naibu waziri wa Kilimo David Silinde wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Hai, ambapo amesema kuwa tayari serikali imemwandikia mwekezaji barua na inaendelea kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu ili kuhakikisha ujenzi wa kiwanda hicho unatekelezwa kwa mujibu wa makubaliano.
Awali Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe alihoji bungeni Dodoma akitaka kujua mpango wa serikali wa kutatua mgogoro uliopo kati ya mwekezaji na Chama cha Ushirika cha Mrososangi ili kuhakikisha masharti ya mkataba yanatekelezwa kikamilifu.