Boma Hai FM
Boma Hai FM
15 May 2026, 11:50 am

Bodaboda watakaobadili taa na milio ya pikipiki kukiona
Na Oliva Joel
Hai-Kilimanjaro
Maafisa usafirishaji maarufu bodaboda wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wameaswa kutokubadilisha mifumo ya milio na taa iliyowekwa katika pikipiki zao na kuweka taa zenye mwanga mkali pamoja na kuweka milio yenye kelele kwani watakapobainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Wito huo umetolewa Mei 15, 2026 na Sajent Ramadhan Juma kutoka katika kituo cha polisi Bomang’ombe kitengo cha usalama barabarani alipokuwa akizungumza kupitia Redio Boma Hai Fm katika kipindi cha Siku mpya.
Amesema kuwa kelele hizo zimekuwa adha kwa wananchi na watumiaji wengine wa barabara huku akiwataka wale ambao wammebadilisha mifumo hiyo kuirejesha katika hali ya kawaida kwani watakaobainika kukiuka agizo hilo watachukuliwa hatua kisheria ikiwa ni pamoja na faini na kupelekwa mahabusu .
Hata hivyo amewaasa madereva kuzingatia sheria za barabarani ili kuhakikisha kuwa wanakuwa salama wao wenyewe na watumiaji wengine wa barabara.