Boma Hai FM

Wilaya ya Hai yapamba moto utekelezaji wa miradi ya maendeleo

5 August 2026, 4:15 pm

Kwenye Picha ni viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Hai wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Hai pamoja na Naibu waziri wa Elimu namfunzo ya amali Zanzibar na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa U.W.T Taifa Hadija Salum Ally (katikati) na mwenyekiti wa U.W.T wilaya ya Hai Happyness Eliufoo (Kushoto) Picha na Henry Keto)

Wilaya ya Hai imepongezwa kwa kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa ubora unaotakiwa huku Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Hai wakiaswa kuendelea kudumisha na kuilinda amani ya nchi

Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Hassan Bomboko amesema Wilaya ya Hai inaendelea kushuhudia maendeleo makubwa kutokana na uwekezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

‎Akizungumza katika mikutano wa umoja wa wanawake wa chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Hai August 4,2026 Bomboko amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuielekezea Wilaya ya Hai fedha za maendeleo, akitaja ujenzi wa miundombinu ya barabara unaoendelea na uliokamilika pamoja na ujenzi wa masoko makubwa ya kisasa, ikiwemo Soko la Kwasadala lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 11 na Soko la Mula lenye thamani ya shilingi bilioni 1.

‎Aidha wilaya ya Hai inaendelea kuwa salama na yenye utulivu na kwamba kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo yanayoshuhudiwa wilayani Hai huku ushirikiano uliopo kati ya viongozi wa Serikali, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi umeifanya Hai kuendelea kusonga mbele kwa kasi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko
Pichani ni Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa U.W.T Taifa Hadija Salum Ally (katikati) akipewa zawadi na wanachama wa U.W.T wilaya ya Hai (Picha na Henry Keto)

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Hai, Happyness Eliufoo, amesema wilaya ya Hai inaendelea kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia wananchi kwa weledi na kuhakikisha huduma bora zinapatikana kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.

‎Eliufoo amebainisha kuwa wanawake wa Wilaya ya Hai wameendelea kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri inayotolewa bila riba, hatua ambayo imewawezesha wanawake wengi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na changamoto ya mikopo yenye riba kubwa maarufu kama “kausha damu”.

Sauti ya Mwenyekiti wa U.W.T wilaya ya Hai Happyness Eliufoo
Pichani ni wanachama wa U.W.T wilaya ya Hai (picha na Henry keto)

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji U.W.T  CCM Taifa ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hadija Salum Ally amepongeza hatua kubwa ya maendeleo inayopatikana katika Wilaya ya Hai pamoja na utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

‎Amewataka viongozi na watendaji kuendelea kusimamia kwa uadilifu fedha za miradi ya maendeleo ili kuhakikisha zinaleta matokeo yaliyokusudiwa na kutimiza malengo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwaletea Watanzania maendeleo na ustawi.

Sauti Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji U.W.T  CCM Taifa ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hadija Salum Ally