Boma Hai FM
Boma Hai FM
14 May 2026, 3:33 pm

Ili kuendelea kufuga kwa tija na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja, wafugaji wametakiwa kuzingatia taratibu na kanuni za ufugaji.
Na Anasta Urio
Hai- Kilimanjaro
Wafugaji wa Nguruwe wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufata kanuni na taratibu za ufugaji zinazotolewa na wataalamu wa mifugo ili Kuwaepusha na magonjwa kwa lengo la kufanya ufugaji wenye tija.
Hayo yamebainishwa afisa mifugo wilaya ya Hai Jackson Ishengoma wakati akizungumza na Radio Boma Hai Fm kwenye kipindi cha siku mpya Mei 14 ,2026 alipokuwa akitoa elimu kuhusu ugonjwa wa homa ya nguruwe.
Ameeleza kuwa ugonjwa wa homa ya nguruwe ni hatari kwani unaua kwa haraka kutokana na virusi ambao wanaambukiza kutoka kwa wanya wa pori kuja kwa wanyama wa kufugwa na ugonjwa huo hauna chanjo hivyo ni vyema wafugaji kuwa makini zaidi.
Aidha amesema kuwa kuna dalili zinazoweza kuonekana kwa nguruwe mara baada ya kupata ugonjwa huo ni pamoja na kuharisha damu,kutapika,mimba kutoka ,na Nguruwe kukosa nguvu ya kutembea hali inayoweza kusababisha kifo kwa nguruwe.
Pia amesema kuwa ugonjwa huo unambukizwa kwa njia ya hewa na kuchangia chakula hivyo amewaasa wafugaji kuzingatia usafi na usalama wa chakula cha nguruwe na ikitokea ili kuwaepusha nguruwe kupata Ugonjwa huo.