Boma Hai FM

Kalanje: Walimu shule za msingi kuzeni michezo shuleni

12 May 2026, 11:51 pm

Pichani ni waalimu wa Shule za msingi wakati wa uzinduzi wa mashindano ya michezo marufu kama Mitashumta (Picha na Henry Keto)

Waalimu wa shule za msingi wilaya ya Hai wameaswa kukuza na kuibua vipaji vya wanafunzi mashuleni ili kujenga timu bora kwaajili ya mashindano ya kimkoa

Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro

Waalimu wa michezo mashuleni wametakiwa kujitoa kuinua na  kukuza michezo katika wilaya ya Hai, ikiwa ni Moja ya sifa muhimu kwa walimu wa michezo mashuleni.

‎Wito huo umetolewa May 11,2026, na Mkuu wa idara ya Elimu ya awali na Msingi Musa Kalanje Wakati wa ufunguzi wa michezo (mitashumta) ilitofanyika katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Hai day, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, ambapo amewataka kuibua na kukuza michezo katika wilaya ya Hai na sio kuangalia tu upande wa Shule yake inayoshiriki kwenye michezo hiyo.

Sauti ya Mkuu wa idara ya Elimu ya awali na msingi Musa kalanje

Pia amesema lengo la michezo hiyo ni kuunda timu ya wilaya itakayoshiriki na kuleta matokeo mazuri katika michezo kwenye ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro, hivyo katika kuendesha mashindano hayo lengo liwe kuunda timu bora na sio kuangalia wanafunzi wa Shule au kata anayotoka peke yake, na hairuhusiwi kuingiza watu wengine tofauti na wanafunzi maarufu kama (Mamluki).

Pichani ni Mkuu wa idara ya elimu ya awali na msingi wilaya ya Hai Musa Kalanje akizungumza na waalimu wakati wa uzinduzi wa mashindano ya michezo marufu kama Mitashumta (Picha na Henry Keto)

Kwa upande wake Afisa michezo wilaya ya Hai Faston Kagimbo ametoa wito kwa walimu ambao wapo kwenye Kamati ya kuunda timu nzuri kuangalia wale wenye uwezo wakuwakilisha mkoa kimichezo na asitokee mwalimu wakuhusika kuchagua mwanafunzi asiye na uwezo kwenye mashindano.

Sauti ya Afisa Michezo Wilaya ya Hai Faston Kagimbo
Pichani ni wanafunzi wa Shule za msingi wakati wa uzinduzi wa mashindano ya michezo marufu kama Mitashumta (Picha na Henry Keto)