Boma Hai FM

Siha yavuka lengo ukusanyaji mapato

7 December 2023, 2:05 pm

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Siha Mh Dankan Urassa wakati wa kikao cha baraza la madiwani Siha

Halmashauri Siha imevuka lengo la makusanyo ya mapato kwa kukusanya bilioni 8.24 robo ya mwaka.

Na Elizabeth Mafie

Halmashauri ya wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imefanikiwa kuvuka lengo kwa kukusanya shilingi bilioni 8.24 katika robo ya Kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Hayo yemebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Dankan Urassa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.

Dankan amesema kuwa halmashauri hiyo imeshika nafasi ya pili kimkoa katika ukasanyaji wa mapato jambo ambalo wao kama madiwani wanaona jitihada za Mlmkurugenzi pamoja na watumishi wengine.

“Kwa hiyo nimpongeze mkurugenzi mtendaji na timu yake, tumeanza vizuri kwani tumevuka lengo la ukasanyaji wa mapato robo ya kwanza”

Amesisitiza kuongezwa nguvu na mikakati katika vyanzo vya mapato ambavyo ukasanyaji wake hauridhishi ili kuhakikisha kuwa halmashauri ya wilaya ya Siha inakusanya mapato yote stahiki kwa mujibu wa sheria ili kuendelea kufanya vizuri katika robo ya pili ya mwaka wa fedha.

“Kkuombe mkurugenzi mtendaji uongeze nguvu na mikakati kwa maeneo ambayo ukasanyaji wake wa mapato uko chini ili kuhakikisha kuwa mnakusanya mapato yote stahiki kwa mujibu wa sheria na robo ya pili mfanye vizuri zaidi”

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Siha Dkt Haji Mnasi amesema kuwa wataendelea kukusanya mapato kwa ufanisi pamoja na kuweka mpango mkakati katika vyanzo vya mapato ambavyo havifanyi vizuri.

Katika Kikao hicho Dkt Haji ameeleza kuwa Halmashauri hiyo imepatiwa zaidi ya shilingi Bilioni mbili kwa ajili ya kuendeleza Miradi ya maendeleo ,ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali ya wilaya,ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi na Sekondari, na mabweni kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.