Boma Hai FM

Siha watakiwa kusheherekea sikukuu kwa amani

25 December 2023, 9:54 am

Mkuu wa wilaya ya Siha Dkt Christopher Timbuka akizungumza katika mbio za Siha marathon (picha na Bahati Chume)

Wananchi wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro watakiwa kusheherekea sikukuu za Christmass na mwaka mpya kwa amani na utulivu.

Na Elizabeth Mafie

Mkuu wa Wilaya ya  Siha mkoani Kilimanjaro  Dkt Christopher Timbuka amesema wamejipanga kuhakikisha usalama wa raia na mali zao katika kipindi hiki cha sikukuu ya Christmass na mwaka mpya ili wananchi waweze kusherea kwa amani na utulivu.

 Dkt Timbuka ametoa  angalizo kwa wale  watakaosherekea kwa kuvunja sheria watapumzishwa kwa muda mpaka pale sikukuu  zitapokwisha na kuwasihi viongozi wa vijiji kuhakikisha vikundi vya ulinzi shirikishi vinafanya kazi ipasavyo  katika msimu huu wa sikukuu.

Akizungumza Mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Siha Marathon yaliyofanyika viwanja vya Fuka wilayani humo,amesema wamejipanga kuhakikisha sikukuu zinasherekewa  bila vikwazo vyovyote na kuwakumbusha wananchi kutumia kila kitu kwa kiasi .

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Siha Dkt Christopher Timbuka.

Kwa upande  wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Dankan  Urasa amewashukuru waandaajj wa mbio hizo ambazo zimekuwa na mchango katika kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu.