Boma Hai FM
Boma Hai FM
12 June 2026, 4:00 pm

Serikali mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa wilaya ya Hai na Chama cha Ushirika FONRWA,uliodumu kwa miaka 23.
Na Anasta Urio
Hai-Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 23 wilaya ya Hai Kata ya Machame Kaskazini baina ya wananchi wa kitongoji cha Lambo Estate na chama cha ushirika FONDWA.
Hayo yamejiri Juni 11, 2026 wakati Babu akiwa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi na vyama vya ushirika Katika ukumbi wa shule ya msingi Nshara kwa lengo la kutoa ufafanuzi wa mgogoro uliokuwepo baina ya wananchi na chama cha ushirika cha FONRWA .

Ameeleza kuwa mgogoro huo umechukuwa muda mrefu na Uongozi wa Ofisi ya mkoa na wilaya wamepambana kwa dhati kuhakikisha umepatiwa utatuzi na ametoa wito kwa wananchi hao kutokuanzisha tena migogoro ya arshi kwani maeneo yaliyotolewa ni kwaajili yao na familia speech zao na sio kwa ajili ya biashara.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko amesema kuwa kutatuliwa kwa mgogoro huo ni hatua muhimu yakuleta maendeleo katika wilaya ya Hai.
Aidha Kamishina wa ardhi mkoa wa Kilimanjaro Rehema Mdee amesema kuwa serikali ya jamuhuri ya muungano Tanzania inalenga kujenga jamii yenye amani ,utulivu na ushirikiano ili kuleta mawasiliano mazuri katika jamii ili kuleta maendeleo kwa taifa.
Pia Mwenyekiti wa chama cha ushirika Cha FONDWA Godwin Nkya amesema kuwa mgogoro huo umechukuwa muda mrefu na amewashukuru wanaushirika wenzake na viongozi wote walioshiriki katika kutatua mgogoro huo na amewaomba wananchi kutokuibua migogoro tena kwenye jamii.
Nae diwani wa kata ya Machame KaskaziniTrael Mboya ameishukuru serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na ushirikiano uliotolewa na pande zote mbili akitoa rai kwa wananchi kwenda kutumia maeneo waliyopewa kwa manufaha yao na vizazi vijavyo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliopata mgao wa mashamba hayo wameishukuru serikali kwa kuwapatia maeneo hayo kwani yatawasaidia katika kuendeleza familia zao na kuomba yale yaliyokubaliwa mahakamani yakasimamiwe vyema.
