Boma Hai FM
Boma Hai FM
25 September 2026, 7:38 pm

Na Gervas Mosha na Salma
“Nimewataka wananchi kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekaji wa nguzo za umeme, kwani fedha tayari zimetengwa na mkandarasi ameshapatikana kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa miradi hiyo.”— Hassan Bomboko, Mkuu wa Wilaya ya Hai.
Wananchi wa kijiji cha Mijongweni, kata ya Mnadani, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya huduma za umeme kupitia TANESCO pamoja na juhudi za kuboresha upatikanaji wa maji, wakisema hatua hiyo imeleta unafuu na kuboresha maisha yao.
Wananchi hao wametoa shukrani hizo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya mnadani ambapo mkuu wa wilaya alikuwa akisikilza kero na kutatua hapo kwa hapo

Katika mkutano huo mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko, amewataka wananchi wa kijiji cha Mijongweni kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekaji wa nguzo za umeme. Aidha, amesema fedha tayari zimetengwa na mkandarasi ameshapatikana kwa ajili ya kuanza kwa miradi ya umeme katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo, ikiwemo kijiji cha Mijongweni.
Kuhusu changamoto ya maji inayowakabili wananchi wa kijiji hicho kwa muda mrefu, Mkuu wa Wilaya ameiagiza MUWASA kufika eneo hilo na kukagua miradi ya maji ili kubaini changamoto zilizopo na kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu.
Naye Diwani wa kata ya Mnadani, Mhe. Emmanuel Mgonja, amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Hai kwa kutembelea kijiji hicho, huku akieleza changamoto na mahitaji ya maboresho katika baadhi ya miradi iliyopo katika eneo hilo.
