Boma Hai FM
Boma Hai FM
1 October 2026, 5:40 pm

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Omary Bomboko amemkabidhi rasmi ofisi Mkuu mpya wa Wilaya ya Hai, Rukia Zuber, baada ya kuhamishiwa wilaya ya Mwanga.
Na Elizabeth Mafie
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Hassan Omary Bomboko, amemkabidhi rasmi ofisi mkuu wa wilaya ya Hai Rukia Zuber, kufuatia uhamisho wake kwenda Wilaya ya Mwanga.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Oktoba 1, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Bomboko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kulitumikia Taifa katika wilaya ya Mwanga.
Bomboko amesema ataendelea kufanya kazi kwa bidii, huku akiahidi kutumia nafasi hiyo kuwatumikia wananchi na kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu.