Boma Hai FM

Wananchi wajulishwe juu ya miradi inayotekelezwa

6 October 2026, 8:58 pm

Pichani ni viongozi mbalimbali walioshiriki katika katika uzinduzi wa jengo la ofisi ya TAKUKURU wilayani Hai,(Picha na Gervas Mosha)

“Wananchi wa Wilaya ya Hai wanapaswa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kutoa thamani iliyowekwa.”— Crispin Francis Chalamila


Na Henry Keto, Gervas Mosha, Teras Munishi

Hai- Kilimanjaro

Wananchi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wameaswa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha pesa zinazotengwa kwaajili miradi ya maendeleo katika Halmashauri zao zinatumika kwa malengo na thamani zilizo wekwa.

Pichani ni Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Crispin Francis Chalamila katika uzinduzi wa jengo la ofisi ya TAKUKURU wilayani Hai,(Picha na Gervas Mosha)

‎Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Crispin Francis Chalamila katika uzinduzi wa jengo la ofisi ya TAKUKURU wilayani Hai, Uliofanyika Oktoba 6, 2026 ikiwahusisha watumishi wa Umma viongozi mbalimbali wa Halmashauri wilaya ya Hai, vyama vya wanafunzi vya kuzuia na kupambana na rushwa.

Sauti ya Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Crispin Francis Chalamila

Sambamba na hilo amewaasa kila Halmashauri ikaweka utaratibu wakuwatangazia wananchi wake miradi yote iliyopitishwa ili wananchi wajue, kuifahamu na kuifuatilia miradi.

Sauti ya Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Crispin Francis Chalamila

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Hai Rukia Ally Zuberi amemshukuru Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mradi huu akisema mradi huu unaenda kuchochea maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Hai.

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Rukia Ally Zuberi akizungumza katika uzinduzi wa jengo la ofisi ya TAKUKURU wilayani Hai,(Picha na Gervas Mosha)

‎Naye Mkuu wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro Musa Chaulo amesema ofisi hii wilayani hai itasaidia kukabiliana na changamoto za Rushwa wilayani hapo na pia ameongelea kuhusu mapambo dhidi ya Rushwa mkoani Kilimanjaro.

Sauti ya Mkuu wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro Musa Chaulo

Jengo hilo la ofisi ya TAKUKURU wilayani Hai limekamilika mnamo mwezi Juni 2026 huku likiwa na gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 400 huku ujenzi ukikamilika na kubaki zaidi ya Milioni 2 zikiwa hazijatumika