Boma Hai FM
Boma Hai FM
1 October 2026, 6:53 pm

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Hai Rukia Zuberi akizungumza na watumishi halmashauri ya wilaya ya Hai (hawapo pichani )mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko (kushoto)pamoja na mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka (picha na Elizabeth Mafie)
Mkuu mpya wa wilaya ya Hai Rukia Aly Zuberi, ameanza rasmi majukumu yake wilayani Hai mara baada ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika Oktoba 1, 2026.
Na Elizabeth Mafie
Na Terasi Munishi
Mkuu mpya wa wilaya ya Hai Rukia Aly Zuberi amekabidhiwa rasmi ofisi na kuahidi kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa wilaya hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
Rukia amekabidhiwa ofisi hiyo Oktoba 1 2026, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, baada ya kuhamishwa kutoka wilaya ya Mwanga.
Amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Hassan Omary Bomboko, aliyekuwa Mkuu wa wilaua ya Hai na ambaye sasa amehamishiwa Wilaya ya Mwanga.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi, Rukia ameshukuru kwa makabidhiano mazuri na kuahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Hai kwa ushirikiano, uadilifu na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya wananchi.