Orkonerei FM

Wakulima Lobosoit wajiandaa kukabili mvua za El Niño

2 October 2026, 1:53 pm

Picha ya baadhi ya wananchi Wa kijiji cha Lobosot wakizungumza na mwandishi wetu (picha na Evanda Barnaba)

Tunaweka dawa kwenye mifuko na kuhifadhi chakula kwa ajili ya watoto na familia zetu. Tunakumbuka miaka ya nyuma kama 1997/1998 kulikuwa na mvua nyingi za El Niño, na wale waliojiandaa vyema waliepuka changamoto kubwa za ukosefu wa chakula,

Na Dorcas Charles

Wakulima na wakazi wa kijiji cha Lobosoit kata ya Emboret Wilayani Simanjiro wameanza kuchukua hatua mbalimbali za tahadhari ikiwemo kuhifadhi nafaka na chakula majumbani mwao ili kujiandaa na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na utabiri wa mvua kubwa za El Niño.

Wakizungumza kufuatia tahadhari za mvua hizo, wakazi na wakulima wa eneo hilo,wameeleza kuwa wametumia mbinu walizofundishwa na maafisa kilimo wa kata pamoja na wadau wa maendeleo. Mbinu hizo ni pamoja na kuweka dawa kwenye magunia ya nafaka na kuyahifadhi kwenye stoo maalum ili kuzuia kuharibika mapema.

Sauti ya wananchi wa kijiji cha Lobosoit.