Orkonerei FM

Wanawake Terrat wahimizwa kushiriki uchumi jumuishi

15 October 2026, 12:03 pm

Picha ya Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Terrat Simanjiro Donald Mpelo akizungumza na mwandishi wetu (picha na Evanda Barnaba)

Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Terrat, Donald Mpelo, anatoa wito kwa wanawake wa jamii ya kifugaji kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika uchumi jumuishi kuelekea Dira ya 2050, huku akikemea mila na desturi zinazowakandamiza. Sikiliza sauti kamili hapa chini.

Na Dorcas Charles

Wanawake wa jamii ya kifugaji hususan kutoka Kata ya Terrat wametakiwa kujitokeza kwa wingi na bila woga ili kutoa mchango wao katika ujenzi wa uchumi jumuishi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Akizungumzia na Orkonerei Fm Radio, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Terrat wilayani Simanjiro, Donald Mpelo, amesema kuwa mfumo wa uchumi utafanikiwa iwapo kila mwananchi atapewa nafasi ya kutoa mawazo yake bila kuachwa nyuma au kusemewa na wengine.

Aidha, jamii imetakiwa kuacha mila na desturi zilizopitwa na wakati zinazowakandamiza wanawake, kwani maendeleo ya nchi yanahitaji ushiriki thabiti wa kila mtu bila ubaguzi.

Sauti ya afisa maendeleo kata ya Terrat Donald Mpelo