Orkonerei FM

Mama mjamzito apigwa nusura ujauzito utoke

13 March 2024, 7:56 pm

Sehemu ya majeraha ya zamani kwenye mkono wa Bi.Penina Milya mkaazi wa kijiji cha Loswaki aliyepigwa na mumewe Bw.Milya Lemesaya. (Picha na Evender Barnaba)

Ukatili wa kijinsia bado unaendelea kuwa tishio kwa maisha ya wanawake wengi hasa kwenye jamii ya kimaasai, kufuatia vipigo kutumika kama sehemu ya adhabu inayotumiwa na baadhi ya wanaume wa jamii hii kwa wake zao.

Na Joyce Elius.

Bi. Penina Milya ambae ni binti wa miaka 24 amenusurika kifo mara kadhaa kufuatia vipigo kutoka kwa mumewe Bw. Milya Lemesaya katika makala haya yaliyoandaliwa na mwanahabari wetu JOYCE ELIUS,Bi.Penina anaeleza kuwa ilifika wakati akatamani kunywa sumu kufuatia mateso hayo.

Naye msaidizi wa kisheria kutoka Shirika la Kiraia la Usaidizi wa Kisheria wilaya ya Simanjiro – SELA, Bi. Scholar Robert anashauri nini jamii ifanye ili angalau kupunguza unyanyasaji huu wa kijinsia kwa wanawake.

Fwatana na JOYCE ELIUS mwanzo mpaka mwisho wa makala hii.