Orkonerei FM

Kauli ya mkuu wa mkoa wa Arusha kuhusu watoto kurejea shuleni

11 January 2024, 1:15 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuweka swala la elimu kuwa kipaumbele na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri na kuhakikisha wazazi wanawapeleka watoto shule.

Na Nyangusi Olesang’ida

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wazazi na walezi wa mkoa huo kuhakikisha wanafunzi wote wanaandikishwa shule na kuwataka wazazi kuwajibika kwa nafasi yao kwani tayari serikali imewajibika kwa nafasi yake

Mongella ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara yake yakutembelea na kukagua maendeleo ya shule katika mkoa huo

hiyo ni sauti ya mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella

kwa upande wa diwani wa kata ya Olmotonyi halmashauri ya Arusha (Arusha dc) Devid Kinisi amewasihi wazazi na walezi kuwa na ushirikiano mzuri na walimu ili kusaidia maelewano katika ulipaji wa chakula shuleni na kuwataka wanafunzi kuwasili shule walizopangiwa hata na sare za shule zile za msingi.

sauti ya diwani kata ya Olmotonyi Devid Kinisi

Baadhi ya wazazi wa mkoa huo wamewashauri wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule na kuwaomba walimu kufanya mawasiliano na wazazi kabla ya kuwarudisha wanafunzi kwasababu ya michango.

baadhi ya wazazi wa mkoa wa Arusha wakizungumza na mwandishi wetu

Naye mwalimu Elifasi Laizer anasema ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora anawasihi walimu na wazazi kuwa na ushirikiano

sauti ya mwalimu Elifasi Laizer