Orkonerei FM

MAKALA:Jinsi uchangiaji damu ulivyo na faida kwako mchangiaji.

15 June 2023, 9:19 am

Mtaalamu wa afya akimsaidia mcangiaji damu katika kuchangia damu siku ya Damu Salama Duniani tarehe 14 juni 2023.(picha kwa msaada wa mtandao).

Kuchangia damu kunafaida si kwa wale wanaokwenda kusaidiwa kwa ile damu uliyochangia lakini pia kwako mchangiaji,kwani unapata namba na cheti cha kuonesha kuwa ni mchangiaji damu kitakachokufanya utambulike kama mchangiaji damu.

Na Isack Dickson

Kila tarehe 14 ya kila mwaka dunia inaadhimisha Siku ya Damu Salama na mwaka huu wa 2023 pia ilifanyika jijini Dodoma kitaifa na mgeni rasmi kuwa Waziri wa afya Ummy Mwalimu ambapo maadhimisho ya mwaka huu yalibebwa na kaulimbiu isemayo “Changia Damu,Changia Mazao ya Damu ,Changia mara kwa mara”.

Je unafahamu ni hatua zipi hufuatwa ili kuchangia damu ? Na wewe umewahi kuchangia damu ? fuatana na mwanahabari wetu ISACK DICKSON katika makala habari hii ili kufahamu zaidi kuhusu hali pia ilivyo ya uchangiaji damu nchini.