Orkonerei FM

Wananchi tafuteni hatimiliki za ardhi kupunguza migogoro

10 July 2024, 3:37 pm

Na Isack Dickson.

Wananchi wa kijiji cha Terrat na wanajamii kwa ujumla wametakiwa kuhakikisha wanamiliki hati miliki za ardhi ili kupunguza migogoro ya ardhi katika jamii.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Terrat Ndg Kone P Medukenya katika mahojiano na mwandishi wetu Isack Dickson Ofisini kwake.

Ndg.Medukenya amesema kuwa migogoro ya ardhi inakwamisha maendeleo mno na ili kupunguza migogoro hiyo basi kila mmiliki wa ardhi ahakikishe anakuwa na hati.