Orkonerei FM

Simanjiro: Terrat waomba muda zaidi ujazaji fomu za maombi ya NIDA

15 January 2024, 3:52 pm

Ofisi ya Kijiji cha Terrat Wilaya ya Simanjiro. Picha na Joyce Elius.

Zoezi la siku tatu la ujazaji fomu za kuomba namba za Kitambulisho cha Taifa-NIDA limekamilika katika kata ya Terrat wilaya ya Simanjiro huku wananchi wengi wakishindwa kujaza fomu hizo kutokana na msongamano.

Na Joyce Elius.

Zoezi hilo la ujazaji wa fomu za maombi ya utambulisho-NIDA limefanyika katika Ofisi ya Kijiji cha Terrat wilayani Simanjiro huku wananchi kutoka vijiji vyote vya Kata ya Terrat(Loswaki, Engonongoi na Terrat) wakijumuika kushiriki zoezi hilo la siku tatu.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Terrat wameomba serikali kuongeza muda na vituo vya kuchukulia fomu za maombi ya namba za NIDA ili kuepusha msongamano na wingi wa watu katika kituo kimoja kama ilivyotokea wakati wa zoezi la awali ambapo ofisi ya Kata Terrat ilitumika kama kituo.

Sauti ya Wananchi wa Kata ya Terrat.

Naye mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Terrat Bw Mosses Abraham Sanago ameishukuru serikali kwa zoezi la ujazaji wa fomu za maombi ya namba za NIDA na kuomba kuongeza muda wa kujaza fomu hizo kwani wananchi wengi wanahitaja vitambulisho vya NiDA.

Sauti ya Mosses Abraham.

Mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Bw Kone Peneti Medukenya ameomba serikali kuongeza muda wa kujaza fomu za kupatia vitambulisho vya NIDA kwani wananchi wasio na Vitambulisho vya NIDA ni wengi katika kijiji cha Terrat na vijii vingine vya Kata ya Terrat.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Terrat.