Orkonerei FM

CCM ARUSHA YATOA PONGEZI KWA RAIS SAMIA

17 March 2022, 9:48 pm

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha na Wilaya ya kichama Meru imepongeza Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Wilayani Arumeru.

Pia.kamati hiyo imemshukuru Mhe.Rais mbali na kutoa zaidi ya bilioni 2.5 za maendeleo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru aliunga mkono ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kikatiti uliosimama toka mwaka 2013 kwa kuchangia kiasi cha Milioni 10 alipokuwa akiwasalimu Wananchi wakati wa ziara yake Mkoani Arusha.

Vilevile Kamati hiyo imemshukuru Mhe.Rais kwa kuteua Viongozi na Watendaji wazuri ambapo wamempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya kwa kujali maslahi ya wananchi ambapo Halmashauri hiyo imetoa Milioni 10 kuchangia ujenzi huo sambamba na kuhamasisha wadau ambao wameahidi kuchangia ujenzi huo ,Pia Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt.John Pallangyo amechangia Milioni 5 kupitia mfuko wa Jimbo.

Akiongea katika ziara hiyo ya kukagua miradi
mbalimbali inayoendelea katika halmashauri hiyo mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Arusha Robert Kaseko amempongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM unaowaletea Wananchi maendeleo katika Sekta ya Elimu,Afya nk ambapo amehimiza Mhe.Rais anaupendo na Wananchi na aliguswa na shida ya wananchi wa Kikatiti na kuchangia milioni 10 katika ujenzi wa zahanati hiyo Oktoba 2021 lakini amewapa mkurugenzi ambaye ana msukumo mkubwa wa shughuli za kiutendaji hasa katika kufuatilia na kusimamia miradi ya serikali inayotekelezwa katika halmashauri hiyo.

“Madiwani na viongozi wengine wote mkimtumia vizuri Mwl. Zainabu 2025 Wananchi watapata maendeleo yaliyokuwa yamekusudiwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM kwani Mwl.Zainabu anajua namna na wapi pa kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi, angoji fedha zinazotoka serikalini tu peke yake na kama mnavyoona ndani ya muda mfupi ametafuta mdau ambaye endapo mambo yatakaa vizuri atamalizia kituo hiki” Amesema Kaseko

Vilevile ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru ikisimamiwa na Mwenyekiti Mhe.Jeremia Kishili kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Vyumba vya Madarasa ambapo ameelekeza miundombinu hiyo kutunzwa ilikuwa na tija zaidi ,Pia .Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa ujenzi wa Kituo cha Afya Maroroni kupitia fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo ambapo mpaka sasa imetoa Milioni 200 na ujenzi wa Jengo la OPD na Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto unaendelea.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili amesema mafanikio ya Halmashauri hiyo ni kutokana na ushirikiano ulipo baina yao na kuahidi kuendelea Kutekeleza Ilani Ya CCM oliyojikita kuwaletea Wananchi maendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amemshukuru Mhe.Rais Samia kwa kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Kikatiti ambapo umeamsha hari ya ujenzi wa zahanati hiyo kwani baada ya Halmashauri kuchangia Milioni 10 na Mbunge Milioni 5 wadau wameahidi Kishiriki kwenye ukamilishaji wa Zahanati hiyo.