Orkonerei FM

Mkopo kwa waendesha Bodaboda Arusha

9 March 2022, 10:03 pm

Na nyangusi Olesan’gida .

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda amezindua Ofisi ya waendesha pikipiki (Bodaboda) katika Kata ya Kaloleni.

Akizindua Ofisi hizo Mkuu wa Wilaya amewataka vijana kuendelea kuheshimu alama za barabarani sambamba na kutotumia pikipiki zenye adha kwa wananchi pamoja na kutotumia taa za rangi katika pikipiki hizo.

Katika Hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Arusha Mrisho Mashaka Gambo amewaahidi vijana hao kuendelea kuwatafutia mikopo nafuu isiyo na riba.

Pia amewahakikishia waendesha bodaboda hao kuwa bado fedha zile zaidi ya milioni mia mbili (200,000,000) zipo kwenye akaunti na yupo kwenye mpango kazi wa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kuweza kuwatafutia mzabuni atakayewapatia pikipiki za bei nafuu.