Orkonerei FM

Umeme jua unavyotumika katika  ushoroba wa Kwakuchinja

8 February 2024, 12:58 pm

Licha ya hatari inayokumba ushoroba wa Kwakuchinja lakini bado kuna jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa ushoroba huo unalindwa na kuendelezwa kwa manufaa ya wanyamapori na jamii zinazozunguka.

Na Isack Dickson.

Ushoroba wa Kwakuchinja ni sehemu muhimu ya makazi na mapitio ya wanyamapori kati ya hifadhi mbili za Taifa za Tarangire na Ziwa Manyara.

Ushoroba huu umekuwa ukitishiwa na shughuli za binadamu zisizo endelevu kama vile uwindaji haramu, ukataji miti, uchomaji mkaa na uvamizi wa makazi ya wanyamapori.

Hali hii imesababisha kupungua kwa idadi na aina ya wanyamapori katika ushoroba huu na kuhatarisha mfumo mzima wa ikolojia. Ili kufahamu zaidi fuatana na mwanahabari wetu ISACK DICKSON katika makala.