Orkonerei FM

Uzinduzi soko la kijiji cha Engonongoi wilaya ya Simanjiro

20 February 2024, 3:28 pm

Wamama wa jamii ya kimasai wakinunua bidhaa mbalimbali kwenye soko la Engonongoi wilaya ya Simanjiro. Picha na Baraka Ole Maika.

Wakaazi wa kijiji cha Engonongoi iliyopo kata ya Terrat wilaya ya Simanjiro wameungana na wananchi wenzao na wafanyabiashara kutoka vijiji vya wilaya ya Simanjiro na wilaya za jirani katika ufunguzi wa soko katika kijiji cha Engonongoi.

Na Baraka David Ole Maika.

Tukio hilo la kihistoria katika kijiji cha Engonongoi lilifanyika jana Jumatatu Februari 19, 2024 katika kitongoji Loordekes katika kijiji cha Engonongoi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama, serikali, makanisa na viongozi wa mila kutoka ndani na nje ya kata ya Terrat.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa soko hilo litakalokuwa likifanyika kila siku za Jumatatu, mwenyekiti wa kijiji cha Engonongoi Bw. Nemamiyai Shinini amesema kuwa kuanzishwa kwa soko hilo itawezesha wananchi kupata huduma kwa karibu kwani wamekuwa wakienda umbali mrefu kwa ajili ya minada.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Engonongoi, Nemamiyai Shinini.

Naye mwenyekiti wa CCM kata ya Terrat ndugu Soipei Koromo amewasihi viongozi wa kijiji cha Engonongoi kuwapa kipaumbele akinamama kwa kuwapatia maeneo ya kufanyia biashara katika soko hilo.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM kata ya Terrat, Soipei Koromo.

Aidha mgeni rasmi katika ufunguzi wa soko hilo diwani wa kata ya Terrat mh Jackson Materi amesema kuwa soko hilo ni fursa kwa wakazi wa kijiji cha Engonongoi na vijiji vya jirani.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Terrat, mh Jackson Materi

Soko hilo la kijiji cha Engonongoi linatazamiwa kuwaunganisha wafanyabiashara na wananchi kutoka kata za Terrat, Oljoro namba 5, Emboreet za wilaya ya Simanjiro pamoja na kata ya Lemooti, Lokisale na Moita za wilaya ya Monduli.

Diwani wa Kata ya Terrat(anayepiga simu) akiwa na mwenyekiti wa CCM kata ya Terrat Soipei Koromo(Mwenye kofia ya CCM), mwenyekiti wa kijiji cha Engonongoi Nemamiyai Shinini(katikati) pamoja na wananchi wa kijiji cha Engonongoi. Picha na Baraka David.