Orkonerei FM

Wajane na mradi wa ufugaji wa ndama.

12 March 2022, 2:48 pm

Ndama 16 ambao ni faida baada ya ufugaji wa kunenepesha.

HABARI.

NA NYANGUSI OLE SANG’IDA.
Kikundi Cha kinamama wajane Noondomonock Sara benk ambacho kipo kata ya Esilalei Kijiji Cha Esilalei leo wamegawana Ndama 16 Ambazo ni faida walioipata baada kikundi hicho kufanya Shughuli za ufugaji na unanepeshaji.

Kikundi hicho Cha wajane ambacho kinalelewa na kusimamiwa na shirika lisilo la kiserikali la Maasae solar chini Mkurugenzi shirika Hilo Ndg.Kisiok Moitiko Leo wameweza kugawana faida walioipata ya ndama16 zoezi Hilo kugawanya Ndama hao wa Ng’ombe limefaywa na Mgeni rasmi katika Shughuli hiyo ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya ya Monduli Bi. Rose Mhina.

Mradi wa kuwawezesha vikundi vya kinamama chini Mradi wa Sara benki ambavyo vipo Katika wilaya ya Monduli,Longido na Ngorongoro
Vimeweza kuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake huku wamama wa jamii ya kifugaji wameweza kubadilisha maisha Yao binfsi na kuwa na Nguvu uchumi katika ngazi ya familia.

Zoezi Hilo limeweza kuhudhuriwa Wananchi pamoja viongozi mbalimbali,Diwani wa kata ya Selela Mh.Richard Paulo,Diwani viti Maalumu Tarafa ya Manyara Mh.Napir na Diwani Tarafa ya Manyara Mh.Mery Lengoije ambaye ni Mratibu wa vikundi vya Sara benki ukanda bonde la Ufa.